Sunday, October 25, 2020

JINSI CONTE ALIVYOMFUNIKA GUARDIOLA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

LONDON, England


KOCHA Antonio Conte anaonekana kuwa ndiye aliyeibuka mshindi dhidi ya mwenzake, Pep Guardiola, licha ya Chelsea  kukosa bahati kabla ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Manchester City  katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Etihad.

Matokeo hayo yanakifanya kikosi cha Mwitaliano kuendelea kutesa kileleni mwa msimamo wa ligi na huku Guardiola  akiendelea kuumiza kichwa kutokana na kipigo hicho cha kwanza akiwa nyumbani tangu alipokabidhiwa mikoba majira ya joto.

 

Katika makala haya, BINGWA litajaribu kukuchambulia jinsi vita ya makocha hao ilivyokuwa na ni yupi aliibuka mshindi.

*Upangaji wa timu

Makocha wote wawili walifanya mabadiliko ambayo hayakutarajiwa kutokana na kuwa na majeruhi.

Kwa upande wa Man City, Raheem Sterling,  aliondolewa dakika za mwisho na  Guardiola akaamua kumpanga,  Leroy Sane,  ikiwa ni mechi yake ya kwanza kuanza katika muda wa wiki sita na huku Chelsea ikimpumzisha, Nemanja Matic ambaye anasumbuliwa na misuli ya nyama za paja na nafasi yake ikachukuliwa na Cesc Fabregas, naye ikiwa ni mara ya pili kucheza kikosi cha kwanza kwenye Ligi Kuu tangu timu hiyo iwe chini ya  Conte.

Pia Guardiola aliamua kuiga mfumo wa  Chelsea kwa kuacha mabeki watatu nyuma ambapo alimuacha benchi Bacary Sagna  huku akiwatumia Sane na Jesus Navas  kama mabeki wa pembeni ili kuwabana  Victor Moses na Marcos Alonso.

*Mshindi

Guardiola 6.5/10

Conte 7.5/10

 

 *Vita ya ufundi

Mbinu za Man City zilifanya kazi kipindi cha kwanza wakati walipomiliki mpira kwa muda mrefu na kufanikiwa kupata bao ambalo Chelsea walijifunga wakati Gary Cahill akiwa katika harakati za kuzuia krosi iliyochongwa na  Navas.

 

Vile vile katika kipindi hicho Man City  walikuwa wakionekana wangepata penalti nyingi lakini zikakataliwa huku bao la kichwa lililofungwa na Fernandinho  likakataliwa kwa madai alikuwa ameotea na pia ikashuhudiwa, Kevin De Bruyne shuti lake likigonga mwamba wa goli.

Pia unaweza kusema siku hiyo, David Luiz, alikuwa na bahati kubwa uwanjani wakati alipoweza kuzuia shuti la  Aguero  wakati Muargentina huyo alipoweza kuwahi mpira wa pasi hafifu iliyorejeshwa nyuma na Cesar Azpilicueta katika kipindi hicho cha kwanza.

Hata hivyo, kama alivyokwishaonywa  Guardiola kwamba vijana hao wa Conte ni wabaya kwa kufanya mashambulizi ya kushtukiza na hawahitaji nafasi nyingi ili waweze kufunga mabao na hivyo ndivyo ilivyotokea na wakaweza kupachika mabao matatu kipindi cha pili kupitia kwa Diego Costa baada ya kukimbilia pasi ndefu ilichongwa na  Fabregas na  Willian akafunga kwa staili hiyo  na kisha  Alonso  akamtangulizia tena pande,  Eden Hazard  aliyefunga la tatu.

 

*Mshindi

Guardiola 7/10

Conte 8/10

 

*Ubadilishaji wachezaji

Mabadiliko muhimu kutoka kwa  Conte  yalifanyika chini ya dakika tano za kipindi cha pili kwa kumwingiza Willian  na kumpumzisha Pedro. Kabla ya mchezo huo nyota huyo wa zamani  wa  Barcelona alikuwa ameshasifiwa na kocha wake wa zamani  Guardiola kwa umahiri wake lakini siku hiyo hakuuonesha.

Kwa upande wake Willian, kwa haraka alionekana kulitatua tatizo hilo baada ya kumzidi mbio beki wa kushoto, Aleksandar Kolarov na kuipachikia Chelsea bao la pili.

Conte pia alilazimika kufanya mabadiliko mengine dakika za mwisho wakati alipomtoa Costa na  nafasi yake ikachukuliwa na Nathan Chalobah na huku  Batshuayi alipoingia kuchukua nafasi ya Hazard dakika za mwisho kama kupoteza muda.

Kwa upande wake Guardiola alijaribu kubadili hali ya mchezo dakika  ya 69 kwa kumwingiza, Gael Clichy, ili akachukue nafasi ya Sane, lakini  pamoja na kuingia beki huyo, haikuwazuia Chelsea kupata bao la pili kutokea upande huo wa kushoto alipokuwa akicheza nyota huyo.

Mbali na beki huyo mabadiliko mengine yaliyofanywa na Guardiola ni kumwingiza Yaya Toure ili akachukue nafasi ya Ilkay Gundogan na hatua ya kumwingiza straika, Kelechi Iheabacho, ili akachukue nafasi ya beki,  John Stones, nayo haikuwazuia  Chelsea kupata bao la tatu.

 

 *Mshindi

Guardiola 5/10

Conte 7.5/10

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -