Thursday, October 29, 2020

Jinsi Ferguson alivyosajili makipa Man United

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MANCHESTER, England

DE Gea ni mmoja wa wachezaji waandamizi wa kikosi cha Manchester United hivi sasa, alijiunga mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid, wakati huo akiwa na miaka 20 na kufanikiwa kucheza kwa miaka miwili chini ya Sir Alex Ferguson kabla ya kustaafu.

Ferguson alifanikiwa kununua makipa wengi kwa kipindi cha miaka 26 aliyokuwa Manchester United. Lakini wapo waliofunika kwa viwango vizuri na wengine kubuma.

Makala haya yanakuletea makipa ambao walisajiliwa na kocha huyo wa zamani raia wa Scotland ambaye aliweka rekodi ya kushinda mataji 13 ya Ligi Kuu England.

Jim Leighton (1988-91)

Leighton alimfuata Ferguson kutoka Aberdeen baada ya kufanya kazi kwa miaka miwili ndani ya timu hiyo. Kipa huyo raia wa Scotland alishindwa kutamba ndani ya kikosi cha Manchester United, kiwango alichokionesha kilipelekea kuwekwa benchi kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la FA mwaka 1990.

Les Sealey (1990-91, 93-94)

Alisajiliwa kuchukua nafasi ya Leighton akitokea Crystal Palace. Sealey alionyesha kiwangoc cha juu huku akiwa mmoja wa wachezaji waliocheza dhidi ya Barcelona katika mchezo wa Super Cup mwaka 1991. Nyota huyo alifariki mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 43, bado anakumbukwa na mashabiki wa Manchester United. 

Peter Schmeichel (1991-99)

Anatajwa kuwa kipa bora wa muda wote wa Manchester United, Schmeichel alishinda mataji 11 akiwa na kikosi hicho, ukijumlisha na makombe matatu waliyoshinda msimu wa 1998/99. Hata alipojiunga na Manchester City kabla ya kustaafu haikuweza kufuta ufalme wake ndani ya Old Trafford.

Tony Coton (1996)

Alitambulika zaidi kama kocha wa makipa ndani ya Manchester United, Coton hakuwahi kucheza hata mmoja ndani ya timu hiyo ya Mashetani wekundu, lakini alitambulika kama kipa bora zaidi alipokuwa Watford na Manchester City. 

Raimond van der Gouw (1996-2002)

Alisajiliwa kama mbadala wa Coton, hata hivyo aliishia kuwa chini ya Schmeichel na baadae Fabien Barthez. Lakini kipa huyo alionyesha kiwango kizuri kila alipopata nafasi kikosini na kufanya timu hiyo kuwa na makipa wenye uwezo mkubwa kwa wakati wote.

Nick Culkin (1997-2002)

Nick Culkin, Kipia wa Manchester United

Alisajiliwa kutoka York City, Culkin aliweka rekodi ya kucheza dakika chache zaidi katika mchezo wake wa kwanza ndani ya Ligi Kuu England, aliingia kutokea benchi dhidi ya Arsenal kabla ya mechi hiyo kumalizika.

Mark Bosnich (1989-91, 1999-01)

Baada ya kuonyesha kiwango kizuri nje ya klabu hiyo, Bosnich alisajiliwa tena kurithi mikoba ya Schmeichel mwaka 1999. Alishinda taji la Ligi Kuu England lakini hakuwa katika kiwango kizuri na kupelekea kuuzwa na Ferguson.

Massimo Taibi (1999)

Taibi aliigharimu Manchester United kitita cha pauni milioni 4.5, kiasi kikubwa cha fedha wakati huo. Taibi alionyesha kiwango kizuri katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya wapinzani wao wakubwa, Liverpool lakini alikuwa kituko kwenye kichapo cha mabao 5-0 walichokipata kutoka kwa Southampton na Chelsea.

Fabien Barthez (2000-04)

Mshindi wa Kombe la Dunia na kikosi cha Ufaransa mwaka 1998, Barthez alikuwa na kipaji kikubwa na mwepesi kufanya maamuzi lakini alikuwa na makosa mengi langoni. Alishinda taji la Ligi Kuu England mara mbili, hata hivyo, hakuwa mchezaji ambaye alitarajiwa na mashabiki wa kikosi hicho.

Roy Carroll (2001-05)

Ukilitaja jina la Roy Carroll, moja kwa moja utakumbuka kuhusu Pedro Mendes. Mshindi wa taji la Ligi Kuu na Kombe la FA akiw na Manchester United anakumbukwa kwa makosa aliyoyafanya dhidi ya Tottenham na kubaki kwenye kumbukumbu kwa mashabiki wa mabingwa hao wa zamani wa Ulaya.

Ricardo (2002-05)

Katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Blackburn Rovers, Ricardo aliruhusu bao na kuokoa mchomo wa penalti, lakini Manchester United walishinda mabao 3-1 mechi hiyo. Tangu hapo hakufanikiwa kucheza kwa kiwango kikubwa tena mpaka anaondoka Old Trafford.

Luke Steele (2002-06)

Alisajiliwa kutoka Peterborough United, lakini Steele hakucheza michezo mingi Manchester United, muda mwingi alitumika katika kikosi cha akiba au kukaa benchi. Kiwango bora alienda kukionyesha Barnsley alikoenda kwa mkopo na kuuzwa jumla.

Tim Howard (2003-07)

Alikuwa chipukizi aliyeonyesha matumaini, Howard hakuwa na muda mzuri Manchester United, hakuonyesha ubora mkubwa na alifanya makosa yaliyopelekea Porto ya Jose Mourinho kusonga mbele Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hata hivyo, alikuwa kipa mzuri Everton na timu ya Taifa ya Marekani.

Edwin van der Sar (2005-11)

VALENCIA, SPAIN – SEPTEMBER 29: Edwin Van der Sar of Manchester United reacts during the UEFA Champions League group C match between Valencia and Manchester United on September 29, 2010 in Valencia, Spain. Manchester United 1-0. Manchester United 1-0. (Photo by Manuel Queimadelos Alonso/Getty Images)

Iliwachukua miaka sita, hatimaye Manchester United walipata mrithi sahihi wa Schmeichel. Van der Sar anaingia kwenye kundi la makipa bora kuwahi kuvaa jezi ya mabingwa hao wa mara nyingi nchini England, alishinda mataji manne ya Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Dunia klabu na mengine.

Tomasz Kuszczak (2006-12)

Kipa mwingine wa Manchester United ambaye alifungwa na kuokoa mchomo wa penalti katika mchezo wake wa kwanza. Muda mwingi alicheza pale Van der Sar alipopumzishwa au majeruhi. Alifanikiwa kushinda mataji saba na kikosi hicho cha Mashetani wekundu.

Ben Foster (2005-10)

Alijiunga na Manchester United kutoka Stoke City, lakini majeraha ya goti yalimfanya apotee na maisha yake ndani ya Old Trafford kuzidi kuwa magumu. Kipa mzuri ambaye aliondoka na kwenda kujiunga na West Brom na Watford.

Anders Lindegaard (2010-15)

Football – Manchester City v Manchester United FA Cup Third Round – Etihad Stadium – 8/1/12 Manchester United’s Anders Lindegaard celebrates Mandatory Credit: Action Images / Carl Recine Livepic

Alitegemewa zaidi wakati De Gea aliposhindwa kuonyesha kiwango kizuri katika michezo ya Ligi Kuu England, Lindegaard alishinda taji la Ligi Kuu msimu wa 2012/13, hata hivyo hakucheza michezo mingi na aliamua kuondoka.

David de Gea (2011 -)

Alishindwa kuonyesha kiwango kizuri alipojiunga na klabu hiyo, lakini De Gea baadae alikuwa tegemeo na kutajwa kuwa mmoja wa makipa bora duniani. Miezi 18 iliyopita, alishindwa kuonyesha kiwango kizuri lakini tangu kuanza kwa msimu huu ameonyesha kurejea kwenye ubora wake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -