Sunday, November 29, 2020

JITAMBUE KATIKA NDOA YAKO ILI MAJUKUMU YAKO ASIPEWE MWINGINE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA RAMADHANI MASENGA,

TATIZO letu kubwa ni kwamba tunapenda sana kulaumu. Ni wachache baada ya kufanyiwa makosa hukaa chini na kujiuliza kwa kina kwanini wahusika wamewakosea hivyo. Wengi ni lawama tu.

Unaamini katika uhusiano wako unatimiza majukumu yako ipasavyo? Unachotakiwa kuleta unaleta na unachotakiwa kuondoa unaondoa? Simanzi nyingi katika majumba ni kwa sababu ya wengi kushindwa kutimiza majukumu yao. Mume hafahamu majukuu yake kwa kina na mke pia hajui afanye nini kaweza kutimiza majukumu yake.

Ndiyo, kuhudumia nyumba ni majukumu yako ila si hayo tu. Je, mke wako ana furaha na amani. Katika furaha na amani yake umeichangia kwa asilimia ngapi?

Kama mume; je, unamfanya mke wako ajihisi ni mwanamke aliye katika ndoa hasa au unamfanya kuwa mama fulani aliye katika jumba fulani na mwanamume fulani?

Kama mwanamume, kuna jambo la msingi unatakiwa kufanya katika nyumba yako. Mke wako ni rafiki na mwandani wako. Amani na furaha yake inapaswa kuanzia katika mikono na maneno yao.

Unamfurahisha inavyopaswa? Kila anachotakiwa kupata anapata? Mbali na kumhudumia kwa kila mahitaji ya kifedha, ila majukumu yako mengine huwa unayatimiza?

Pale katika mkutano wenu wa usiku unamfanya ajihisi wa pekee na kuona thamani ya kuwa na wewe? Siungi mkono usaliti hata siku moja, ila najua wengi wanaosaliti huwa na sababu zao. Japo za kipuuzi ila zina maana kama utaamua kuzisikiliza kwa makini.

Kama unamfanyia mambo ilimradi unadhani atakuwa na amani na furaha? Wewe ukija unamaliza tu shida zako kisha unageuka pembeni au unachukua laptop na ubize unaanzia hapo! Maisha hayo  atavumilia mpaka lini?

Mke wako anahitajika afurahi, ajidai na kuona ile thamani ya kuwa na wewe katika ndoa. Na abadani vitu hivyo haviwezi kupatikana ikiwa hutimizi majukumu yako ipasavyo.

Mke, mume wako ana amani na furaha kwa sababu yako? Au na wewe kila kitu hujui na hata hutaki kujifunza? Fanya kitu kwa ajili ya furaha na mpenzi wako. Mumeo ni rafiki na mwandani wako hasa.

Mpe furaha na amani ili aione thamani ya kuwa na wewe katika uhusiano. Siyo kila kitu hujui. Maneno machafu kama ulivyo mwili na nguo zako. Maana yake nini? Jua majukumu yako. Wewe ndiye mtawala wa nyumba.

Waziri mkuu wa chumba, kila jukumu la usafi na pambo la nyumba liko chini yako. Iko vipi nyumba yako? Uko vipi mwili wako? Katika ule mkutano wenu mahususi na mume wako, hali huwaje? Ni furaha au ilimradi liende? Shauri yako.

Huwezi kuwa na amani katika uhusiano wako kama humfanyi mwenzako ajihisi wa thamani na bora katika maisha yako na yake. Kwa kila jambo unalotakiwa kufanya, hakikisha unalifanya katika ubora unaotakiwa.

Si kila muda upo upo tu. Nguo si safi, nyumba chafu, mwili wako hata hautamaniki! Unadhani atajivunia kuwa na wewe?

Japo kila siku tunakemea usaliti na upuuzi katika uhusiano, ila wengi mambo hayo mnayaleta wenyewe. We mchafu, una kauli za hovyo na bado hujiweki katika mazingira ya kumfanya mpenzi wako akakuhitaji, unadhani atakuwa anakuwaza wewe tu?

Acha kulalamikia tabia ya mwenzako. Jiangalie kwanza na wewe. Wengi mnaleta mabalaa katika nyumba zenu wenyewe. Hamjitambui wala hamjui mnatakiwa kufanya nini katika majumba yenu. Hapo mambo unadhani yatakuwa vipi?

Tambua majukumu yako. Kila mtu akijua majukumu yake katika nyumba hakuna huzuni zilizokuwapo zitakazobaki. Mke majukumu yako si kufua na kupika tu. Mume  majukumu yako si kununua chakula na kusomesha watoto tu. Yapo zaidi ya hayo. Kuwa makini ili uweze kuyatekeleza vizuri.

          ramadhanimasenga@yahoo.com

Previous articleUPENDO KUSHINDA UFAHAMU [112]
Next articleREFA WAO
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -