Tuesday, November 24, 2020

Jiulize haya kabla ya kutaka kurudiana naye

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

IMEANDIKWA kwamba, mwenye kusamehe kwa kosa alilofanyiwa na mwenzake, huwa ni kipenzi cha Muumba. Kwa kuwa Mungu ni mwingi wa kusamehe, humfurahia binadamu mwenye tabia hii.

Mbali na mambo mengine, ila mtu mwenye kusamehe hujionesha katika jicho la Muumba kuwa hakuna binadamu aliyekamilika na kwa kuwa hata yeye (binadamu ambaye husamehe) hajakamilika, basi husamehe na wengine kwa sababu binadamu wote tunateseka kwa mapungufu yetu.

Asili ya mtu ambaye hasamehi ni kiburi, hujionesha yeye ni bora na ambaye hukosea basi ni mjinga. Hii ni dhana mbaya si tu mbele ya Mungu, bali hata katika maisha ya kawaida.

Kwa sababu mtu mwenye dhana hii atakuwa katili na hata kuweza kuleta maafa kwa wengine, kwa sababu katika kichwa chake humwona mkosaji kama mtu ‘ziro’ kabisa.

Huu ndio ukweli kuhusu mtu ambaye hapendi kusamehe wengine. Ila ukweli huu haunajisi ukweli mwingine kuwa kuna watu huwa wanakosa sifa ya kusamehewa hivyo hawapaswi kusamehewa.

Kama Mungu mwenyewe kaumba pepo na moto, na kaufanya moto kuwa makazi ya watu watukutu ambao watakosa sifa za kusamehewa, wewe ni nani kuamini kila mtu anastahili msamaha? Kuna watu hawastahili kusamehewa.

Katika suala la mahusiano ya mapenzi, hoja hii tuijadili katika namna pana kiasi. Kwanza tuijadili kuwa mtu anaweza kukukosea sana na hata kufikia hatua ya kukudhalilisha kinamna fulani, ila ukaamua kumsamehe kutokana na namna alivyokushawishi kuwa hawezi kurudia ujinga wake na kuendelea naye katika maisha.

Hapa msamaha huwa unaangalia zaidi majuto ya mhusika na ushawishi wake kuwa kajifunza na jambo alilofanya alilifanya kutokana na kukosa uelewa katika mambo fulani fulani. Kwa hoja hii, mtu anaweza kusamehewa na kuendelea kuwa pamoja katika maisha.

Ila pia unaweza kuamua kumsamehe mtu, yaani kuamua kutomchukia wala kukumbushia madhila aliyokufanyia katika maisha na kuamua kuendelea na maisha yako bila yeye. Hii inatokana na namna nafsi yako unavyoiona.

Yaani mbali na msamaha  na mapenzi unayohisi bado unayo kwa mhusika, ila huamini kama anaweza kuwa mpenzi bora kwako ama huamini kama unaweza kuwa na amani ukiwa naye. Kwa hoja hii unaamua kusamehe ila uhitaji tena mahusiano naye ya kimapenzi katika maisha yako.

Si vema kukurupuka kumrudia mtu bila kujiuliza maswali magumu kabla ya kuwa naye. Ujuzi wake wa kimapenzi, mwonekano wake ama ‘kutakata’ kwake kimaisha kusiwe kigezo cha kusema sasa ngoja niwe naye. Ukifanya hivyo si tu unakaribisha mashaka katika maisha yako, ila pia jua unaiuza furaha yako kwa bei rahisi sana.

Kama anataka kurudiana na wewe, jiulize ni sababu gani zilifanya mkatengana mwanzo. Sababu hizi zipo ama zimeisha? Jiulize, kama alikukosea wewe, kafanya jambo gani kukuaminisha kuwa anajutia makosa yake na anastahili tena msamaha na kuweza kuwa pamoja na wewe? Ila mbali na yote, jiulize, una amini utakuwa na furaha na amani ukiwa naye?

Hautokuwa na mashaka wala hofu juu ya matendo yake? Kama ukiwa na hofu, jua hajakushawishi vya kutosha kuwa kabadilika na atakuwa mpenzi bora katika maisha yako. Acha kukurupuka. Maisha yako ni bora sana kuliko uwepo wake wa mashaka.

Wengi wanajutia mahusiano waliyoyarudisha kwa wenzao. Wanajutia kwa sababu wenzao bado wanafanya yale yale yaliosababisha wateseke na kutengana nyakati za nyuma. Kuwa makini na uamuzi wako wa kurudisha makao kwa mwenzako.

Ni vema kuwa na mtu anayekujua na unayempenda kwa dhati. Tena wakati mwingine ni vema zaidi kuwa na mtu ambaye mliwahi kutengana kwa sababu wengi huwa wanajua makosa yao na kukujua vizuri wewe. Ila jiulize ametakata? Hana makosa ya kijinga na matendo yasababishayo maumivu ya makusudi katika maisha yako?

Haina haja kumrudia mtu kwa lengo la kupata amani ila unaona kabisa bado ana mambo yale yale yavunjayo amani katika maisha yako. Wakati mwingine ni vema sana kuwa mwenyewe kuliko kukurupuka kuwa na mtu.

Kuwa na mtu bila kupata amani na furaha  ni hatari sana kwa ustawi wa maisha yako. Amua kwa makini mtu wa kuwa naye bila kuangalia sababu ambazo hazina maana wala msingi katika maisha yako.

Kuna watu waliachana na wenzi wao na kurudiana na leo wanaishi maisha ya raha na amani. Kila wanapokuwa pamoja kila mmoja anajua namna ya kuishi na mwenzake kutokana na kila mmoja kumjua vema mwenzake, kitu kinachosababisha amani halisi katika maisha yao.

Ila wapo wengine baada ya kurudiana na wenzao, mambo yamekuwa mazito katika maisha yao. Ile amani na furaha waliyoitarajia katika maisha yao si tu haipo, bali pia sasa hawajui ni kwanini waliamua kuwa na wenzao. Chaguo ni lako.

Ama umrudie tu kwa sababu umemkumbuka wakati ana matendo yale yale ya ajabu na yakutia fadhaa na mwishowe akupe mateso na karaha. Ama uamue kupambana na upweke wako mpaka wakati maridhawa utakapofika na wewe kuwa na mtu mwenye kujua thamani na hadhi yako katika maisha yake.

    ramadhanimasenga@yahoo.com

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -