Friday, December 4, 2020

JJUUKO AIBUA HOFU SIMBA SC

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA MWANDISHI WETU

BEKI wa kimataifa wa Uganda na Simba, Jjuuko Murshid, amezua hali ya sintofahamu ndani ya klabu ya Wekundu hao kutokana na kutowasili nchini licha ya muda wa mapumziko aliopewa kumalizika.

Murshid alikuwa sehemu ya kikosi cha Uganda ‘The Cranes’ kilichoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) iliyofanyika nchini Gabon na Cameroon kuibuka mabingwa.

Uongozi wa Simba ulimpa beki huyo mapumziko ya siku saba baada ya kutoka kushiriki michuano ya Afcon akiwa na kikosi cha Uganda ambayo iliondolewa katika hatua za awali.

Chanzo kutoka ndani ya klabu ya Simba kimeliambia BINGWA kuwa uongozi wa timu hiyo hauna taarifa kutoka kwa beki  huyo kuhusiana na sababu ya kushindwa kwake kujiunga na wachezaji wengine.

Chanzo hicho kilidai uongozi wa Simba ulijaribu kufanya mawasiliano na beki huyo kwa njia ya simu lakini juhudi zao ziligonga mwamba kutokana na kutopatikana hewani.

“Tumefanya juhudi za kumtafuta kwa simu yake, pia tumemtumia wakala wake lakini na yeye hajampata, hivyo tumewasiliana na Fufa (Shirikisho la Soka la Uganda),” alisema.

Makamu wa Rais wa Simba, Gofrey Nyange `Kaburu`, alipoulizwa kuhusiana na  taarifa hizo alikiri kutoripoti kwa wakati kwa Murshid.

“Jjuuko alitakiwa kuwasili nchini tangu Jumapili ya wiki iliyopita lakini hadi sasa hajawasili na hatuna taarifa juu ya sababu za kuchelewa kwake,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -