Na KYALAA SEHEYE
MKONGWE wa filamu za Tanzania, Blandina Chagula ‘Johari’, amesema yeye pamoja na wasanii walioanzia kwenye vikundi vya uigizaji wamepanga kurudisha heshima ya soko la filamu lililoporomoshwa na wasanii wasio na maadili.
Johari ameliambia Papaso la Burudani kuwa, wasanii walioibuka bila kupitia vikundi vya sanaa ndio waliokuja kuharibu mfumo mzima wa sanaa yao na kujikuta wakipata umaarufu huku wakiharibu sanaa.
“Ikumbukwe kuwa, wasanii tuliopita kwenye vikundi vya sanaa kama Kaole tunaweza kuikuza sanaa katika misingi na maadili, tumegundua wasanii walioibuka wanaharibu sanaa yetu, tumejipanga kuweka sawa heshima ya tasnia nzima,” alisema Johari.