Sunday, January 17, 2021

John Bocco abatizwa jina jipya Simba

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

JOHN

NA EZEKIEL TENDWA

BAADHI ya mashabiki wa Simba, wameridhishwa na uwezo ulioonyeshwa na Straika wao mpya John Bocco, ambaye wapinzani wao walikuwa wakiubeza usajili wake na sasa wamempachika jina jipya la ‘Faru John’.

Bocco alionyesha uwezo mkubwa kwenye mchezo wa kirafiki wa Tamasha la Simba Day, uliochezwa Jumanne wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda, uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Mohamed Ibrahim ‘Mo’ juzi.

Simba wamemsajili Bocco, kutoka Azam FC, lakini wapinzani wao walicheka juu ya usajili wake,  wakiodai wekundu wa Msimbazi  hao  walilamba garasa, lakini uwezo aliouonyesha kwenye mechi hiyo, umewafanya mashabiki hao kutoka uwanjani wakitembea vifua wazi.

Licha ya kwamba Bocco alishindwa kuzitumia vizuri baadhi ya nafasi alizozipata, lakini alifanya kazi kubwa huku akilitumia vema umbo lake kubwa kuwazidi ujanja wachezaji wa Rayon Sports.

Wakizungumza wakati mchezo huo ukiendelea na baada ya kumalizika, baadhi ya mashabiki walisema uwezo mkubwa uliionyeshwa na John Bocco, ni salamu kwa wapinzani wao.

“Walisema Bocco ni garasa sasa wenyewe wamejionea jinsi anavyopambana uwanjani, nadhani hizi ni salamu kwao, kuanzia leo hataitwa tena John Bocco, na badala yake ataitwa Faru John,”, alisema shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Huruma Othmani, huku akiungwa mkono na wenzake.

Mbali na Bocco, pia mashabiki hao walikoshwa na uwezo wa wachezaji wao wote waliosajiliwa akiwamo Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi, Aishi Manula na Erasto Nyoni na wengine.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -