Wednesday, November 25, 2020

Jonas Mkude awapa habari njema Msimbazi

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude, amewatoa hofu mashabiki wa timu  hiyo akiwataka kujitokeza kwa wingi Oktoba Mosi, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, kushuhudia jinsi watakavyoisambaratisha Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mashabiki wa Yanga wamekuwa wakitamba kuendeleza ubabe wao kwa Simba, kama walivyofanya msimu uliopita pale waliposhinda mechi zote mbili kwa mabao 2-0 na mwisho wa siku kutwaa ubingwa wa kipute hicho.

Akitambua tambo hizo za watu wa Yanga, Mkude ameliambia BINGWA kuwa yeye na wachezaji wenzake hawana hofu na Yanga pamoja na mchezo baina ya timu hizo kuwa na presha kubwa, huku ukiteka hisia za mashabiki wengi wa soka hapa nchini na kwingineko.

“Tumejiandaa vizuri, naweza kusema tunatambua mchezo utakuwa mgumu kutokana na wenzetu nao wamejiandaa, ila tunategemea kupata matokeo mazuri baada ya dakika 90 za mchezo,” alisema Mkude.

Mkude amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanjani siku hiyo kuwapa sapoti, akiamini hilo linaweza kutimiza ndoto yao ya kuifunga Yanga na kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo baada ya kuwa wasindikizaji kwa takribani misimu minne.

Kati ya mambo yanayompa jeuri Mkude ni ubora wa safu yao ya ushambuliaji, inayoongozwa na Laudit Mavugo, mshambuliaji mwenye kipaji cha hali ya juu, Ibrahim Ajib, Fredrick Blagnon pamoja na mawinga Shiza Kichuya na Jamal Mnyate.

Mbali ya hao, kikosi cha Simba kimesheheni viungo mafundi kama Mkude, Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla, Muzamiru Yassin na wengineo, huku kwenye beki kukiwa na visiki kama Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Janvier Bukungu, Method Mwanjali, Jjuuko Murushid, Novaty Lufunga na wengineo.

Katika hatua nyingine, Mkude alisema mkataba wake na klabu ya Simba wa miaka miwili aliosaini umebakisha miezi michache kumalizika kabla ya kutoa msimamo wake juu ya majaliwa yake ndani ya klabu hiyo.

“Nimebakiza miezi michache kumaliza mkataba wangu, nikimaliza ndio nitaweka wazi wapi naelekea au nini nataka, lakini kwa sasa siwezi kuzungumzia lolote,” alisema Mkude.

Licha ya kuwepo tetesi za kiungo huyo kutimkia nchini Afrika Kusini kucheza soka la kulipwa, Mkude aliliambia BINGWA kuwa lolote linaweza kutokea mara baada ya kumaliza mkataba wake na Simba.

“Kwa sasa meneja na mkataba unanibana kuzungumzia masuala ya baadaye, lakini pia siwezi kusema kwa sasa thamani yangu ni kiasi gani, ngoja muda ufike nitasema,” alisema Mkude.

Misimu miwili iliyopita, kiungo huyo aliikomba Simba Sh milioni 80 na   kupewa gari aina ya GX 115 ili kukamilisha usajili wake ndani ya kikosi hicho, ikiwa ni baada ya Yanga na Azam kuonyesha nia ya kumsajili msimu wa 2014/15.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -