Monday, November 23, 2020

JOTI: MSIIGE KILA KITU KWA JOTI, HAMTATOKA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA BEATRICE KAIZA

JIACHIE na Staa Wako kama kawaida kila inapofika Jumanne inamsogeza kwako wewe msomaji wa BINGWA staa mmoja wa hapa Bongo.

Katika toleo lililopita tuliahidi kumleta hapa msanii wa sanaa ya vichekesho kutoka kundi la Original Comedy, Lucas Mhavile ‘Joti’.

Jiachie na Staa Wako lilifanikiwa kukutana na Joti na kumbananisha ili aweze kujibu maswali yenu kama mlivyonituma.

Joti ambaye amejipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania kupitia kazi yake hiyo ya uigizaji, amejibu maswali yenu kama hivi:-

Swali: Mwaku wa Kinondoni Studio, Dar es Salaam. Naomba kujua kuhusu Original Comedy, bado ipo au imekufa na kama ipo kwa sasa wasanii wa kundi hilo mnafanya kazi gani.

Jibu: Original Comedy ipo lakini kwa sasa si kundi, bali ni kampuni na inatuingizia fedha hadi leo.

Lakini kutokana na kuongezeka kwa majukumu tumeona si vibaya tukapumzika kwa muda ili kutoa fursa kwa wasanii wachanga kuonyesha kazi zao na sisi tufanye biashara nyingine.

Kwa upande wangu nimeamua kutumia mapumziko yangu kubuni kitu kipya.

Nimeamua kuanzisha TV ya Online ambayo itakuwa inapatikana kupitia Youtube na nimefanya hivyo kwakua dunia ipo kwenye kiganja, unaweza kuafuatilia kazi zangu kwenye simu ukiwa mahali popote na sehemu yoyote.

Swali: Pendo wa Kimara, Dar es Salaam, kwenye mitandao ya kijamii kuna picha zimezagaa zikionyesha wewe na Giggy Money, hatua iliyosababisha watu wahisi ni wapenzi, unazungumziaje hili.

Jibu: Ahahaha! (kicheko), tetesi hizo hazina ukweli wowote, Giggy Money ni rafiki yangu wa kawaida tu.

Swali: Mjuni wa Mwanza, unakutana na changamoto zipi katika kazi yako ya  sanaa ya vichekesho.

Jibu: Nimepitia changamoto nyingi hadi kufikia hapa lakini kubwa ni pale ninapokuwa kazini na kulazimika kuuvaa uhusika, mwanzoni ilikuwa vigumu mashabiki kunielewa.

Pongezi: Mama Suzy wa Kigoma, mimi ni shabiki wako namba moja nakupongeza kwa uchapakazi wako, watoto wangu wanakupenda sana, naomba siku uje huku Kigoma ufanye tamasha ili watoto wangu wakuone.

Jibu: Asante sana, Mama Suzy nitalifanyia kazi na nitakuja Kigoma.

Swali: Glady Samweli wa Ilala, Dar es Salaam. Naomba kufahamu kutoka kwa Joti, amejipangaje katika suala zima la kusaidia vipaji vya wasanii chipikuzi.

Jibu: Napenda kuona vipaji mpya vikiibuka, nimejipanga kuwasaidia wasanii chipukizi kwa kuwapa nafasi ya kuonekana kupitia TV yangu ya Online ambayo inapatikana kupitia Youtube.

Watakuwa wanalipwa kutokana na uwezo wao wa kazi, naomba mashabiki na wapenzi wa kazi zangu wakae mkao wa kula.

Swali: Juma Bakari wa Dodoma, nje ya sanaa unajishughulisha na nini.

Jibu: Nje ya sanaa mimi ni mfanyabiashara.

Swali: Honory Aloyce wa Kilimanjaro, Joti, kwanini unapenda kutoa remix za nyimbo za wasanii wengine?

Jibu: Ni moja ya kazi zangu za sanaa.

Pongezi: Mozes wa Kibaha, Pwani na Habiba wa Morogoro, kwenye tasnia ya uchekeshaji hapa Tanzania sijaona wa kufafana na wewe kwa kipaji cha uigizaji, hongera sana.

Jibu: Asante sana Mozes.

Swali: Amina wa Zanzibar na Rehema Omary wa Handeni, Tanga. Vipi suala la kufunga ndoa nakumbuka tuliona unamvisha pete mchumba wako.

Jibu: Ndoa ni mipango ya Mungu, kama nimefanikiwa kumvisha pete mchumba wangu basi na ndoa ipo njiani.

Swali: Zena Saidi wa Magomeni, Dar es Salaam. Unawashauri nini wasanii wachanga ambao wanatamani kutimiza ndoto zao.

Jibu: Ushauri wangu kwa wasanii chipikuzi, wanatakiwa kuwa wabunifu ili kuleta ladha mpya kwa mashabiki na si kila mtu anafanya kile kile anachofanya Joti.

Sisemi wasifanye kazi ambayo mimi nafanya, hapana, lakini wanatakiwa kuwa wabunifu zaidi ili wapate mashabiki wapya wanaofanya vizuri Tanzania.

Pongezi: Antony Mselewa wa Kondoa. Hongera kaka Joti kwa kazi zuri, pia nakutakia kazi njema yenye mafanikio.

Jibu: Asante sana tupo pamoja Antony.

Hawa ni baadhi ya mashabiki wa Joti, waliojitokeza kumuuliza maswali na kumpa pongezi.

Katika toleo lijalo tunamleta kwenu msanii wa filamu, Wastara Juma.

Wastara anafanya vizuri katika tasnia ya  filamu hapa nchini.

Miongoni mwa kazi  zake zinazotamba ni pamoja na ‘Hapendeki’ na  ‘Faulo’.

Tumia fursa hii kumuuliza maswali ili kukata kiu yako, pia unaweza kumpa ushauri na pongezi kwa kutuma sms kupitia namba ya simu iliyoko hapo juu na majibu yatapatikana hapa hapa katika toleo la Jumanne ya wiki ijayo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -