Saturday, October 31, 2020

JULIO AFICHUA SIRI YA MAVUGO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR

KOCHA msaidizi wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amefichua siri ya mshambuliaji wa timu hiyo, Laudit Mavugo, kuanza kufunga mabao katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mavugo alifunga bao maridadi dhidi ya Majimaji katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Majimaji, wakati Simba wakishinda mabao 3-0 baada ya kuwekwa chini na Julio.

Akizungumza na BINGWA jana, Julio alisema alikutana na Mavugo na wachezaji wengine wa Simba katika kikao maalumu kilichowahusisha nyota wa zamani wa timu hiyo, akiwamo  Zamoyoni Mogella, Abas Kuka, Mtemi Ramadhani, Dua Said na kumpa ujumbe mzito.

Julio alisema alimkalisha chini Mavugo na kumwambia Simba ni timu kubwa,  hivyo matokeo mazuri uwanjani kwa asilima kubwa yanamtegemea na kumtaka mshambuliaji huyo kuamini kuwa Mungu yupo kwa ajili ya kuwasaidia waliomkosea na wale wanaomcha.

“Kwenye mpira lolote linawezekana kama tunavyoamini kuwa Mungu yupo,  tusichoke kumuomba kwani ukimuomba anakupa na ukiomba msamaha kama ulimkosea atakusamehe, ukitambua hilo mambo yako lazima yaende sawa,” alisema Julio.

Julio alimtaka Mavugo kutokata tamaa kutokana na kushindwa kufunga mabao kwenye michezo kadhaa ya ligi kuu na kumtaka akaze, kwani bado ana uwezo wa kuipa matokeo mazuri timu hiyo na kumsisitiza kumcha Mungu.

“Nilikaa nikamwambia kupitwa pointi moja na Yanga wasikate tamaa kwani  ubingwa bado upo kwa Simba, naamini hivyo,”  aliongeza Julio.

Kwa upande wa Laudit Mavugo, amemshukuru Julio kwa nasaha zake nzuri zilizomrudisha mchezoni.

Akizungumza na BINGWA, Mavugo alisema kufanya kwake vizuri kwenye mchezo dhidi ya Majimaji ya Songea kulitokana na nasaha nzito alizopewa na kocha huyo wa zamani wa Simba.

“Kabla ya mchezo alinifuata na kuongea na mimi muda mrefu huku akiniambia uwezo wa kuipa ubingwa msimu huu ninao, hivyo natakiwa nitulize akili nicheze kwa kujiamini mwisho wa siku niipe matokeo timu,” alisema Mavugo.

“Aliniambia ni mchezaji ambaye Simba inanitegemea na ubingwa wa msimu huu upo mikononi mwangu, kwa kweli maneno hayo yalinijenga na kunifanya nijiamini muda wote wa mchezo,” aliongeza Mavugo.

Alisema tangu atue Tanzania hajawahi kupata mtu na kuzungumza naye maneno muhimu kama hayo na kumfanya ajione yeye ni shujaa.

“Ukweli maneno ya Julio yamenijenga na sasa najiona jasiri, naamini nitabadilika na kufunga katika kila mechi ambayo nitapangwa kwenye kikosi cha Simba.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -