Tuesday, October 27, 2020

KAA MBALI NA HILI ILI UFURAHIE UHUSIANO WAKO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA RAMADHANI MASENGA          |           


 

UKWELI ni kwamba kila binadamu ana mapungufu yake. Na kitu cha hatari zaidi ni kwamba, kila mmoja humuona mwenzake ana mapungufu ya ovyo zaidi.

Ila msingi wa kuishi na watu kwa amani na furaha ni kuangalia zaidi mapungufu yako kuliko kuangalia ya kwao.

Kila mtu huwa hajisikii amani akiambiwa mapungufu yake. Hii inatokana na tabia ya kibinadamu ya ubinafsi.

Kila mtu hujiona mjanja, kabarikiwa na mwerevu zaidi. Hali hii inafanya kila mtu kujiona anastahili kukosoa kuliko kukosolewa.

Unaishi vipi katika mahusiano yako? Mahusiano mengi yameingia katika migogoro kwa sababu ya wahusika kujifanya wajuaji, wakosoaji na kupenda kujadili zaidi mapungufu ya wenzao kuliko kufurahia penzi lao.

Ndugu yangu, kama tabia yako ni kupenda sana kujadili makosa ya mwenzako, kusema juu ya namna alivyowahi kukukosea, kujidai unamuongoza sana kwa sababu yeye hajielewi wewe ndiyo unajielewa zaidi, fahamu kuwa unapoteza nafasi ya kufurahia mapenzi na kumfanya mwenzako awe huru zaidi na wewe.

Ili mahusiano yenu yawe na furaha na amani, inabidi mjiachie. Kuna wakati inabidi  msahau kama mliwahi kugombana na kufurahia uhusiano wenu.

Kupenda kukumbushia alivyowahi kukukosea si tu hakufanyi asikukosee, ila pia kunafanya mahusiano yenu yachangamke.

Furaha hutawala pale kunapokuwa na mazingira ya furaha. Kukosoana kila muda hukimbiza mazingira ya furaha.

Kwa sababu hiyo kila siku utajikuta huna amani, raha wala furaha kwa ajili ya penzi lenu.

Mwenzako hawezi kuacha kukukosea kwa kusomewa risala kila siku. Hapana. Mwenzako ataacha kukukosea ukimwambia juu ya kosa lake kwa muda mfupi kisha kutengeneza mazingira ya furaha katika mahusiano yenu.

Mazingira ya furaha, raha na amani ndiyo yatamfanya mwenzako asiweze kukukosea kwa kuhofia kukosa raha na amani ambayo huwa ipo katika uhusiano.

Yafanye mahusiano yako kuwa bora, kwa kumfanya mwenzako afurahi na wewe. Kukosoana kila siku kunamuondolea hata mazingira ya kujiamini mwenzako.

Ukipenda sana kuzungumza anavyokukosea unamtia unyonge katika nafsi yake na hata hatimaye anakuwa hayuko tayari kukaa na wewe muda mrefu.

Hakuna binadamu anayefurahia kukosolewa kila muda. Mtu akiona anakosolewa, mara nyingi uwahama hata watu wamfanyiavyo hivyo.

Tathmini inaonesha hata mwalimu darasani anayependa kuutweza na kuukosoa uwezo wa wanafunzi wake hushusha morali yao na hata na wanafunzi hupoteza hamasa ya kuwa naye darasani.

Maana ya mapenzi ni kupendana kwa dhati na kudekezana. Huenda ni kweli kuna tukio ambalo mwenzako amewahi kukufanyia na linakuuma sana.

Ila kwa afya ya uhusiano wenu na furaha, usipende kulisema sana tukio hilo.

Unaweza kudhani kuwa unapolisema mara kwa mara, mwenzako ndiyo atazidi kuwa bora ila ukweli ni kwamba unapolisema tukio hilo mara kwa mara, unamfanya mwenzako asiwe na furaha wala uchangamfu kwa sababu atajiona mwenye hatia katika nafsi.

Watu katika mahusiano wanatakiwa kuishi kama marafiki. Wakikoseana waambiane ila si kila muda wafundishane na wabwatizane.

Mahusiano ya kufundishana kila muda si tu yanakosa ladha, ila yanawafanya wahusika wayatazame kwa jicho tofauti.

Mahusiano ni raha na amani. Sasa vipi yageuke kuwa darasa la kuchoshana kila siku?

Miongoni mwa watu wasioweza kudumu katika mahusiano yao ni wale wenye kujifanya walimu sana kwa wenzao na wakamilifu sana.

Yaani wenyewe badala ya kufurahia uhusiano wao, wenyewe wako busy kuangali nani kakosea wapi na kwa sababu gani. Mahusiano ya hivyo hayawezi kusonga mbele.

Raha kamili ya uhusiano inapatikana kwa wahusika kujiachia na kila mmoja kujiona yuko na mtu wa sawa yake na si yuko na mtu wa hadhi ya juu zaidi.

Ili furaha ya kweli katika uhusiano itawale, kila mmoja anatakiwa amuone mwenzake ni saizi yake.

Kama mtu akijihisi yuko na mtu wa hadhi ya juu zaidi ama ya chini yake, mahusiano haya yanakosa msisimko.

Na njia nyepesi ya kuepuka tatizo hili, ni kukataa kukosoana ovyo wala kutwezana. Mtu anapokosolewa sana, hujihisi mnyonge, mkosaji ama mjinga.

Hali hii inampelekea kuamini yeye ni wa viwango vidogo na yuko na mtu wa viwango vikubwa.

Fikra hizi zinampelekea kuwa mwoga kutenda, kuongea ama kuwasilisha anayotamani au anayohisi yatamfanya kufurahi ama kumfurahisha mwenzake.

Wapo wanaoishi katika mahusiano kama mtu na baba yake mkwe. Wanaogopana hata kutaniana hakuna.

Mbali na mambo mengi yanayoweza kutokea kwa hali hii, ila kubwa mhusika mnyonge atakuwa na hamu ya mahusiano ya watu wengine kuliko kusisimuliwa na mahusiano yake.

Mwenzako akikosea mwambie ila usiwe wimbo wa kila siku. Penda katika mahusiano yako kuangalia upande wa furaha zaidi kuliko wa matatizo.

Ukipenda kuangalia upande wa matatizo, hata wewe utajikuta unahisi mtu uliye naye hakufai hivyo unahitajika kutafuta mtu mwingine.

Kitu ambacho si sahihi sana. Nani utakuwa naye na akawa sahihi kwa asilimia mia moja?

Mahusiano bora huzidi kujitengeneza kutokana na namna wahusika wanavyoishi.

Instagram: ramadhan.masenga

Mwandishi wa makala hii ni mtaalamu mbobezi wa masuala ya ushauri wa uhusiano, maisha na utulivu wa hisia (Psychoanalyst).

ramadhanimasenga@yahoo.com / +255 719 053 327

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -