Saturday, October 31, 2020

KAJUNA, TULLY, JASMINE WAPINGWA SIMBA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAITUNI KIBWANA

KAIMU Makamu wa Rais wa Simba, Iddy Kajuna na wajumbe wenzake wa Kamati ya Utendaji, Ally Suru, Jasmine Badar Soudy na Said Tully, wamewekewa pingamizi katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika Novemba 3, mwaka huu.

Viongozi hao tayari wamepitishwa kwenye usaili wa kutafuta wagombea watakaoingia kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya timu hiyo.

Akizungumza na BINGWA, mwanachama mwenye kadi namba 00547 kutoka tawi la Mpira Pesa, Said Mohamed ‘Bedui’, alisema amewawekea pingamizi viongozi hao kwa kushindwa kuwasilisha mapato na matumizi kwa miaka minne waliyokaa madarakani.

Alisema wajumbe hao chini ya Rais Evans Aveva na Makamu wa Rais, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, walishindwa kuwasilisha mapato na matumizi kwa kipindi chote huku wakijua ni kosa la kikatiba.

“Kila mwaka katiba ya Simba inasema lazima viongozi watangaze mapato na matumizi, lakini hawa walifanya mara moja tu msimu wa 2015/16 ambapo hata hivyo hesabu zao zilikatawaliwa na wale waliokuwa wakikagua mali za Simba,” alisema.

Katika hatua hiyo, mwanachama Jackson John ‘Chacha’, aliliambia BINGWA ameweka pingamizi kwa ajili ya mjumbe mmoja ambaye hata hivyo aligoma kumtaja.

“Nimeweka kweli pingamizi kwa kuwa ni haki yangu kisheria, ila siwezi kusema nimemwekea nani kwa kuwa hii ni kama mahakama,” alisema.

Licha ya Chacha kugoma kutaja mgombea aliyemwekea pingamizi, habari kutoka ndani ya klabu hizo zinasema amemwekea Mwina Kaduguda.

Kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo inatarajia kuanza kupitia mapingamizi hayo kuanzia Septemba 27 hadi 29, ambapo Oktoba1 ni siku ya kutoa maamuzi ya pingamizi.

Akizungumza na BINGWA, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Steven Ally, alisema zoezi la kupokea pingamizi limemalizika rasmi leo (jana).

“Tulianza kupokea mapingamizi toka Septemba 21 hadi 23, hivyo baada ya hapo tutaanza kupitia moja moja na kuwasikiliza pande zote mbili,” alisema.

Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Novemba 3, mwaka huu licha ya awali kuzuiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Revocatus Kuuli, ambaye hata hivyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limempa siku tatu wakili huyo kujieleza kwanini aliusimamisha uchaguzi huo.

Katika barua iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau, Kuuli ametakiwa kujieleza kama uamuzi wake wa kuusimamisha uchaguzi wa Simba SC umetokana na kikao cha kamati yake cha Dodoma.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -