Friday, September 25, 2020

Kakolanya kumng’oa Manula Stars?

Must Read

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi...

NA SALM MPELI


WAKATI wachezaji Taifa Stars wakiingia kambini, kocha mkuu wa timu hiyo, Emmanuel Amunike, atakuwa na mtihani wa kuendelea kumpanga kipa Aishi Manula, kutokana na kiwango kilichoonyeshwa na Beno Kakolanya katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kati ya Simba na Yanga.

Katika mchezo huo uliochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Kakolanya, alionyesha umahiri mkubwa wa kudaka na kumshawishi kocha wa Stars kuweza kumpanga katika kikosi chake cha kwanza, kinachojiandaa kucheza na  Cape Verde.

Manula ambaye alikuwa chaguo la kwanza la Amunike, huenda akaanzishwa Kakolanya kutokana na uwezo alioonyesha katika pambano la watani.

Taifa Stars wameingia kambini  kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika (Afcon) dhidi ya Cape Verde, utakaochezwa Oktoba 12, mwaka huu, Mji wa Praia.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo, alisema wachezaji wanaocheza ligi ya  ndani wamejiunga kambini  kabla ya kuungana na wale wanaocheza nje ya Tanzania.

Ndimbo alisema mazoezi ya Taifa Stars yanatarajia kuanza leo asubuhi kwenye Uwanja wa JMK Youth Park, jijini Dar es Salaam.

Wachezaji walioitwa kujiandaa na mchezo huo ni Aishi Manula, Salum Kimenya, Frank Domayo, Salum Kihimbwa, Kelvin Sabato, David Mwantika na Ally Abdulkarim Mtoni.

Wengine ni Mohamed Abdulrahiman, Beno Kakolanya,

Hassan Kessy, Gadiel Michael, Abdi Banda, Aggrey Morris, Andrew Vicent, Himid Mao, Mudathir Yahya, Simon Msuva, Rashid Mandawa, Farid Mussa na Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Shabani Chilunda,

Yahya zaydi, Kelvin Yondan, Paul Ngalema, Jonas Mkude, John Bocco, Shomari Kapombe, Feisal Salum na Abdallah Kheri.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu yao ni kuwa na mwendelezo...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi tatu kila mchezo, wakianzia mechi...

CHAMA GUMZO KILA KONA

NA WINFRIDA MTOI KIWANGO kilichoonyeshwa na kiungo wa Simba, Clatous Chama katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu Tanzania...

United ‘kimeo’ yamtoa povu Evra

MANCHESTER, EnglandBEKI wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra, amekerwa na namna mambo yanayoendelea katika klabu hiyo, hasa ishu za usajili.
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -