Saturday, November 28, 2020

KAMA KWELI UNAIPENDA YANGA, WASOME HAWA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR,

SIMBA na Yanga zinatarajiwa kukutana Jumamosi ya wiki hii katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na mambo mbalimbali, zaidi ikiwa ni uhasimu wa timu hizo mbili, lakini pia kutokana na nafasi zao katika mbio za ubingwa, kwani hadi sasa hakuna yenye uhakika wa kutwaa taji.

Homa ya pambano hilo tayari imeanza kupanda kwa pande zote mbili, huku kila moja ikijinasibu kuibuka na ushindi mnono siku ya pambano hilo.

Kuelekea pambano hilo, BINGWA linakuletea makala ya mahojiano maalumu iliyofanya na baadhi ya wachezaji wa Yanga na wanachama wa timu hiyo.

DEOGRATIUS MUNISH ‘DIDA’

Kipa huyo namba moja wa mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Yanga, amesema haoni kikwazo kitakachoizuia timu yao kutetea taji lao, kutokana na kiwango bora wanachokionesha katika michuano yote wanayoshiriki msimu huu.

Akiuzungumzia mtanange wao na Simba, Dida alisema utakuwa mchezo mgumu na wenye presha kwa pande zote mbili, lakini ameipa timu yake nafasi kubwa ya kushinda kutokana na uwezo na vipaji vya wachezaji waliopo kikosini.

Alisema kitakachoifunga Simba katika pambano hilo la Februari 25 ni vipaji walivyokuwa navyo wachezaji wa Yanga na uzoefu wa kucheza mashindano makubwa ukilinganisha na Simba.

VINCENT BOSSOU

Beki huyo ‘katili’ wa Yanga, amesema piga garagaza, siku hiyo Uwanja wa Taifa ‘utaongea’ kwa jinsi alivyopania kuwanyamazisha mastraika wa Simba, Ibrahimu Ajib na Laudit Mavugo.

Bossou alisema siku hiyo hatakuwa na mambo mengi uwanjani zaidi ya kuwapa ‘surprise’ mashabiki, wapenzi na wanachama wa Yanga kwa kuifanya kazi yake kiufasaha zaidi.

“Nimerudi kutoka Gabon, nina maujuzi mapya ya AFCON, sasa sina mengi ya kuzungumza. Uwanja ndio utaongea siku hiyo, tumwachie Mungu kwa kila jambo,” alisema Bossou.

NADIR HAROUB ‘CANNAVARO’

Mkongwe huyu alisema kuelekea katika pambano hilo la Februari 25, hakuna kitakachowazuia kushinda na kuwaomba mashabiki na wapenzi wa Yanga kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwenda kuwapa sapoti.

“Tuna imani ya kufanya vizuri, hakuna mtu wa kutuzuia, Simba tunawafahamu, tunaichukulia kama timu ya kawaida sawa na nyingine, hakuna jipya zaidi ya kuwafunga na kutangaza ubingwa mgongoni mwao,” alisema Cannavaro.

Nyota huyo ambaye pia alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, aliongeza kwamba, pamoja na kuuchukulia mchezo huo kama mwingine, lakini pia wamepanga kupambana kufa au kupona kuhakikisha wanabeba pointi hizo dhidi ya Simba na michezo mingine ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kuwaacha mbali wapinzani wao.

“Kwanza nataka ujue kwamba, huo ni mchezo wa kawaida, pili, wachezaji wetu hawana hofu na mchezo huo kutokana na kwamba wengi wetu wana uzoefu na mechi hiyo, hivyo tumejiandaa kushinda na kutetea taji letu. Simba ndio watakuwa ngazi ya sisi kubeba taji la ubingwa msimu huu,” alisema.

Katika mchezo wa kwanza wa mahasimu hao uliochezwa Oktoba mosi mwaka jana, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Amis Tambwe, kabla ya Shiza Kichuya kuisawazishia Simba kwa mpira wa kona ulioingia moja kwa moja.

SOUD TALL

Huyu ni kati ya wanachama maarufu wa Yanga ambaye amesema kuelekea katika pambano hilo hakuna kitakachowazuia kuwafunga Simba, kutokana na maandalizi kabambe wanayoendelea kuyafanya.

“Kimsingi hakuna kitakachotufanya tusiwafunge Simba, tuna hasira kubwa tangu mwenyekiti wetu apate matatizo hivi karibuni, tumekuwa na hasira mara mbili zaidi,” alisema Tall.

Tall alisema njia pekee ya kumfariji mwenyekiti wao ambaye alipata matatizo hivi karibuni ni kuwafunga Simba zaidi ya mabao matatu, kwani kufanya hivyo itakuwa ndiyo zawadi yao kwa mwenyekiti huyo.

“Zawadi pekee ya kumpa mwenyekiti wetu ni kuwafunga Simba mabao matatu, hakuna kingine, tunajua mengi yanazungumzwa na yanaendelea kuzungumzwa, tunasubiri hiyo siku ifike tufanye kazi yetu,” aliongeza Tall.

MHANDISI PAUL MALUME

Huyu ni mmoja wa viongozi wa Yanga, akiwa ni mhandisi ambapo ndani ya Yanga ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano.

Kuelekea mchezo wa Jumamosi, amesisitiza jambo moja tu kuwa, watake wasitake, Simba lazima wafungwe.

“Tumevurugwa kwa kweli, lakini pamoja na kuvurugwa bado haituzuii kuifunga Simba,” alisema Malume.

Alisema mchezo wao na Simba ni wa kawaida, hivyo hakuna sababu ya vijana wake kuwa na presha.

“Ni pambano la kawaida ambalo halihitaji kuwa na presha, tumejipanga zaidi. Baada ya kamanda wetu kupata matatizo, hali hiyo imetuongezea morali wa kufanya vizuri zaidi,” alisisitiza.

ABAS SHAIBU ‘HEAVY D’.

Mwanachama huyo maarufu wa Yanga tawi la Manzese, amesisitiza kikosi cha Task Force cha Yanga chini ya uongozi wake kimejipanga kuhakikisha ‘mnyama’ anakufa siku hiyo.

“Tumejipanga, ndiyo tulipata matatizo, Mungu kasaidia yamekwisha, kimsingi tumejipanga, hakuna hujuma yoyote itakayotokea siku hiyo ndani au nje ya uwanja,” alisema.

“Naomba vijana wenzangu wote wa Yanga tushirikiane tuweke itikadi zetu kando, tufanye kazi kwa ushirikiano ili ‘mnyama’ aweze kukaa hiyo Februari 25 pale Taifa,” aliongeza.

EDWIN KAISI

Naye hakuwa kando kuelezea namna ‘mnyama’ atakavyouawa siku hiyo na kusema wamejipanga ndani na nje kuhakikisha pointi zote tatu muhimu zinapatikana katika mchezo huo.

“Tunajua utakuwa ni mchezo mgumu, lakini nikwambie kitu, baada ya mwenyekiti wetu kupata matatizo tumekaa na kujadiliana kwa kina juu ya zawadi gani tumpe, tumeona zawadi pekee ni kuifunga Simba, hakuna nyingine,” alisema Kaisi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -