Tuesday, November 24, 2020

KAMA NDOA YA KAZI GANI, NI KWANINI UPO KATIKA UHUSIANO?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NI kweli kuna tofauti kubwa kati ya kuishi katika mahusiano ya kimapenzi (bila ndoa) na kuishi ndani ya ndoa. Ndoa inahitaji umakini na hali ya uthabiti. Watu walio katika ndoa hupaswa kuwa ni wale wenye kukubaliana kwa dhati na hali ya wenzao na hali zao.

Yaani wawe watu wenye kuamini wenzao wana ubora na hadhi mahususi za kuishi na wao. Katika aina hiyo ya fikra maana yake atamuona mwenzake ndiyo hasa anayepaswa kuujua mwili wake na mwenye kupaswa kutunzwa na kuenziwa.

Kwa mtu ambaye akili yake haiko sawa ndoa kwake itakuwa maigizo. Kwa mtu mwenye pupa ni lazima atajuta baadaye katika maisha ya ndoa.

Ndoa ni taasisi muhimu sana kwa maendeleo ya familia na furaha ya kila mtu. Ukiwa na pupa maana yake utaingia kimakosa katika ndoa na matokeo yake hutokuwa na furaha na kupelekea kutofikia lengo la ndoa.

Vijana wengi wanashindwa kumudu ndoa kwa sababu huwa wanapupa na kuangalia sababu dhaifu za kutambua wanaowahitaji katika maisha yao. Akili za vijana wengi wanatazama vitu vya nje na kuamini ndivyo vitakavyowapa amani na raha katika ndoa zao.

Si ajabu kumsikia kijana akisema: “Nikimpata msichana msomi, mzuri na anayefanya kazi, basi nitamuoa na nina amini nitafurahia maisha.” Kwa akili za namna hii ndiyo maana baada ya muda ndoa hugeuka kuwa chungu na huanza kudhani ndoa huwa ni maalumu kwa watu kuanzia miaka 37 na kuendelea. Kitu ambacho si sahihi hata kidogo.

Kuna ndoa nilihudhria ya vijana wadogo. Tangu mwaka 2004 mpaka leo bado wako katika hali ya amani na furaha. Si mara zote umri huwa sababu ya kudumu au kuachana katika ndoa. Ni vizuri zaidi uwe makini ili uweze kugundua ni vitu gani unahitaji katika ndoa.

Wewe ni kijana? Upo katika mahusiano na unaogopa kuingia katika ndoa? Kama ndivyo, ni kwanini upo katika mahusiano?

Mahusiano ya kimapenzi huwa ni njia tu ya kuingia katika ndoa kwa watu makini na wenye kujali maadili.

Ukiwa na mtu katika mahusiano na anahitaji kuwa hivyo kwa muda mrefu bila suala la ndoa maana yake anahitaji zaidi ngono na wewe na wala hana hisia za kweli za kimapenzi.

Jiulize unachohitaji katika mahusiano yako. Zinaa inapoteza heshima na hadhi yako katika jamii. Zinaa inakukimbiza mbali na rehema na baraka za Mwenyezi Mungu. Kwanini unahisi hutaki kuingia katika ndoa?

Kama unahisi muda bado unaweza kukaa mbali na mahusiano na ukafurahia maisha kwa namna nyingine. Najua wengi wanajidanganya kuwa haiwezekani. Na kama unaamini hivi basi huenda kamwe usiweze katika maisha yako. Ila kitaalamu najua fika inawezekana

Ni kujua tu namna ya kucheza na akili na fikra zako. Kudhibiti tamaa za kingono ni vyepesi kuliko kuepusha nafsi yako kupenda. Anayekwambia haiwezekani si kweli ila yeye hajui mbinu mwafaka za kufanya aweze.

Kama nilivyosema awali ndoa inahitaji umakini na utulivu wa kisaikolojia. Akili za kitoto haziwezi kumudu ndoa. Ila kijana mwenye kujua nini anafanya na akapata ushauri wa kina kabla hajaingia katika ndoa, basi ndoa huwa ni furaha na amani ya kila siku.

Ndoa si mbaya ila akili na dhamira mbaya huleta ndoa mbaya. Ukimuoa kwa sababu ya makalio makubwa, jua ukiwa naye utayazoea na kutamani mwenye kitu kingine. Hivyo ndivyo tamaa huwa. Haina mwisho!

Ikiwa unajiona huna shida ya ndoa kwanini unakaa katika njia yake? Mahusiano ni njia ya kuelekea katika ndoa kwa walio ‘serious’ na wenye kujua wanachofanya. Kuwa na boyfriend au Gilfriend si ‘fashion’, kataa kuishi kwa kuiga. Kuwa na mipango na malengo katika maisha yako ya kimahusiano. Ahsanteni!

ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -