Wednesday, November 25, 2020

KAMA YANGA NDO WANGEKUWA 10… Simba SC wangepiga hata bao 7

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba, wameibuka na kusema laiti wapinzani wao, Yanga wangekuwa pungufu kama walivyokuwa wao kwenye mchezo wao wa wikiendi uliyopita, basi wangewapiga hata bao 7-0.

Kauli hiyo imetolewa jana na mashabiki mbalimbali wa soka ambao waliamua kuzungumzia kitendo cha Simba kuwa pungufu na kuweza kucheza kandanda safi kwenye mchezo huo.

Akizungumza na BINGWA, shabiki wa Simba, Ramadhani Wasoo, alisema wapinzani wao, Yanga, walipopata bao la kwanza hawakucheza tena kwa nguvu kama ilivyokuwa awali.

Alisema kitendo cha mahasimu wao hao kupata bao la kwanza waliwadharau na kujua kwamba mchezo umekwisha, ndicho kitu ambacho kiliwaathiri.

“Nawashangaa sana Yanga, yaani tupo pungufu wanashindwa kutufunga, halafu baada ya kupata bao wame-relax na kusahau kuwa kwenye soka lolote linaweza kutokea,” alisema.

Naye shabiki wa timu hiyo kutoka tawi la Mpira Pesa Magomeni, Fii kambi, alisema laiti Simba ndiyo ingekuwa pungufu, basi wapinzani wao wangepigwa hata saba.

“Simba ipo pungufu, imecheza kwa kupambana sana, je, ingekuwa imekamilika kama ilivyokuwa Yanga ingekuwaje, unadhani si wangepigwa hata saba wale,” alisema.

Simba juzi imelazimisha sare ya bao 1-1 na wapinzani wao, Yanga, huku wakisawazisha bao dakika za lala salama, licha ya kuwa pungufu toka dakika ya 27 baada ya nahodha wake, Jonas Mkude, kutolewa kwa kadi nyekundu na mwamuzi Martin Saanya.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -