Tuesday, October 27, 2020

Kamusoko akenua meno 32 Yanga

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SALMA MPELI

KIUNGO wa Yanga, Thabani Kamusoko, amefurahia timu yake kufunga idadi kubwa ya mabao katika mechi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya Kagera Sugar wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kisha mabao 4-0 dhidi ya JKT Ruvu iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA juzi, Kamusoko alisema anafurahi kuona timu yake inafunga idadi kubwa ya mabao katika mechi mbili mfululizo.

Kamusoko alisema wakiendelea kupata ushindi katika mechi itakayofuata dhidi ya Mbao FC, watakuwa wamejiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao.

“Nimefurahi na ushindi wetu dhidi ya JKT Ruvu, lakini pia ni kiwango kizuri na kikubwa kimeonyeshwa na timu yetu kwenye mechi mbili kwa kupata idadi kubwa ya mabao,” alisema.

Yanga kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 24, baada ya kucheza mechi 11 huku Simba wakiwa kileleni kwa pointi 29.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -