Wednesday, October 28, 2020

Kamusoko, Mkude vita ya mafundi Oktoba mosi

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAITUNI KIBWANA

HAKUNA asiyejua kuwa kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko, alisajiliwa kwa hela ndefu tu pale Jangwani akitokea FC Platinum ambapo kuelekea ‘derby’ ya Simba na Yanga, atakuwa na kibarua kizito cha kupambana na  Johas Mkude ambaye alisajiliwa kwa dau la milioni 60 pale Msimbazi.

Viungo hawa wote ni mafundi na wanaweza kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani. Wakicheza nafasi za kiungo mkabaji, wanatimiza majukumu yao vizuri, lakini kwa sasa Mkude anacheza zaidi ya kiungo mkabaji, wakati Kamusoko anacheza kama kiungo mshambuliaji.

Wanajua kupiga vichwa na hata kufunga lakini Kamusoko licha ya kuwa na uwezo mzuri wa kumiliki mpira, ni mchezaji tegemeo na anaweza kuitwa ndiye ofisa mipango wa Yanga anayeunganisha vyema safu ya kiungo na ushambuliaji.

Mkude naye ana uwezo wa kumiliki mpira, anafanya kazi nzuri ya kuwalinda mabeki wake wakati huo akifanya kazi ya kupanga mashambulizi ya timu yake.

Msimu uliopita, vita ya Kamusoko na Mkude haikuwa dhahiri sana hasa kutokana na Yanga kutumia viungo watatu, huku Mkude akikabiliana na Haruna Niyonzima na Kamusoko akionekana kuwa huru zaidi uwanjani.

Mkude na Kamusoko wote wanapiga pasi nzuri, lakini Kamusoko ana miguu mirefu na mepesi mno kutoa pasi, lakini katika ukabaji, Mkude anaonekana yuko vizuri zaidi na ndiyo maana Joseph Omog amekuwa akimtumia kama sentahafu wakati mwingine.

Katika kuchezesha timu, Kamusoko yuko vizuri na ndiyo maana Pluijm amekuwa akimpanga kiungo wa juu mara nyingi.

Wote wakongwe na wamefanikiwa kuwateka mashabiki wa timu zao na hata kuwakuna mashabiki wa upande wa pili, huku kila mmoja akiheshimika kutokana na uwezo wake.

Je nani atamrudishia chenji mwenzake? Ni Mkude atakayeifanya Simba ing’are katika mechi hiyo kama ilivyokuwa katika mechi zilizotangulia, au ni Kamusoko tena ataendelea kutamba kwenye dimba na kuipa Yanga ushindi wa tatu mfululizo mbele ya Simba? Mambo yote ni Oktoba mosi, Uwanja wa Taifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -