Sunday, January 17, 2021

KAMUSOKO, TSHISHIMBI WAMPA DARASA NGOMA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAITUNI KIBWANA

VIUNGO wa Yanga, Thaban Kamusoko na Papy Kabamba Tshishimbi, wamenogesha mazoezi ya timu hiyo yaliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam juzi, kutokana na pasi zao murua zilizomkosha mno mshambuliaji wa timu hiyo, Donald Ngoma.

Kwenye mazoezi hayo, yaliyofanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi sita mchana na kusimamiwa na Kocha msaidizi Shadrack Nsajigwa na Noel Mwandila, nyota hao watatu walionyesha kiwango cha hali ya juu.

Katika zoezi hilo la ufungaji wa kutumia krosi, Ibrahim Ajib, Pius Buswita, Donald Ngoma, Matheo Antony na Yusuph Mhilu, walionyesha umahiri mkubwa wa kuunganisha krosi, licha ya nyingine kuokolewa na kipa, Youth Rostand.

Mara kadhaa Ajib, Ngoma, Matheo na Mhilu waliweza kumtungua kipa huyo na mashuti mengine kuokolewa.

Katika zoezi la mashuti, wachezaji waliong’ara ni Nadir Haroub Canavaro, Buswita, Juma Mahadhi waliweza kumfunga mabao ya ustadi wa hali ya juu Rostand kwenye zoezi lililodumu zaidi ya saa moja.

Baada ya kumaliza mazoezi hayo, Mwandila aligawa vikosi viliwili, cha kwanza na pili na kuwaelekeza namna ya kutengeneza mashambulizi kupitia pembeni kwa mawinga.

Mwandila katika zoezi hilo, aliwataka mabeki au kipa kuanzisha mpira ambapo alitakiwa kuupiga mpira mrefu kwenda pembeni kwa beki wa kulia ambaye naye atarudisha kwa beki wa kati na kuanza kucheza.

Katika zoezi hilo wachezaji Kamusoko, Tshishimbi na Ngoma walionekana kukinogesha vilivyo kikosi cha kwanza kutokana na staili yao ya kuachiana pasi (one, two).

Kamusoko aliwakuna zaidi wapenzi wachache waliohudhuria mazoezi hayo, kutokana na bao lake la kichwa alilolifunga lililotokana na krosi ya Juma Abdul, ambapo kabla ya mpira kumfikia aligongeana vema na wenzake.

Mbali na kufunga bao hilo, lakini pia kiungo huyo aliweza kutengeneza bao lingine lililotokana na mpira wake alioubetua baada ya kumhadaa kipa Rostan na kumkuta Mhilu aliyefunga bao hilo.

Kikosi cha timu hicho kipo kwenye maandalizi makali ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Njombe Mji ya mkoani Njombe, itakayochezwa Jumatano ya wiki ijayo.

Timu hiyo inatarajia kuondoka Jumatatu kwa ajili ya kuwafuata wapinzani wao hao ambao wamepanda daraja msimu huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -