Saturday, November 28, 2020

Kante wa sasa si wa Caen ama Leicester City

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

BAADA ya kufanya vibaya msimu uliopita, Chelsea imerejesha matumaini ya kufanya vizuri msimu huu. Tangu mwanzo wa msimu huu, dimba la Stamford Bridge limekuwa sehemu nzuri ya kushuhudia soka la kuvutia, kitengo cha mitandao ndani ya klabu hiyo, kimejizatiti kwa kuweka picha mnato na video.

Picha hizo zitakufurahisha kuanzia vituko na ushangiliaji wa Kocha Antonio Conte, mabao yaliyofungwa na wachezaji Willian, Kante na Costa.

Chelsea ilianza msimu huu kwa kusuasua na baada ya kocha kufanya  mabadiliko ya kiufundi uwanjani, wachezaji, Eden Hazard amerejea katika kiwango chake na mshambuliaji Diego Costa anaonyesha kufurahia uwezo wake.

Hakika siri kubwa ya mafanikio hayo ni kiungo wa Ufaransa, N’Golo Kante, ambaye ushirikiano wake na Nemanja Matic katika safu ya kiungo, umebadili aina ya uchezaji wa kikosi kizima cha The Blues.

Katika msimu wake wa kwanza nchini England, kiungo huyo ameonyesha uwezo wake hadi kufikia kuteuliwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa FIFA mwaka 2016.

Kiungo huyo wa Ufaransa ndiye mchezaji aliye na uhakika wa namba katika kikosi cha Antonio Conte, kutokana na majukumu aliyonayo.

Katika klabu alizochezea nchini England na Ufaransa, Kante alicheza kama kiungo mkabaji anayetibua pasi za wapinzani, lakini sasa anatakiwa kukaba na kuanzisha mashambulizi.

“Nadhani Chelsea ni tofauti na klabu nilizowahi kucheza, kwa sababu nilipokuwa Caen na Leicester City, hatukumiliki mpira sana na tulifanya mashambulizi ya kushtukiza.

“Ni vizuri kumiliki mpira kuliko kuutafuta.Tulikaba kama timu na ulipofika wakati wa kuutafuta mpira, nililazimika kuwajibika.”

Katika safu ya kiungo, Kante, anashirikiana vizuri na kiungo raia wa Serbia, Nemanja Matic, na ushirikiano wao umetengeneza safu bora ya kiungo katika Ligi Kuu ya England.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -