Monday, August 10, 2020

Kapombe apata pacha

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA WINFRIDA MTOI

KLABU ya Simba imeanza kushusha vifaa vipya, ikianza na beki wa kulia, David Kameta ambaye atakuwa msaidizi wa Shomari Kapombe ambaye kwa muda mrefu amekosa mtu wa kumpa changamoto.

Kameta amesajiliwa na Wekundu wa Msimbazi hao kutoka Lipuli FC iliyoshuka daraja, kutokana na kuonesha kiwango kizuri msimu huu uliomalizika hivi karibuni.

Taarifa ambazoBINGWA imezipata baada ya kusambaa picha ya mchezaji huyo katika mitandao ya kijamii akiwa anasaini mkataba, zinasema kuwa amepewa miaka miwili kuwatumikia Wanamsimbazi hao.

Msimu wa 2019/2020, licha ya kumsajili mkongwe Haruna Shamte, Simba imekuwa ikimtegemea zaidi Kapombe na anapopata majeraha, kunakuwa na hofu ya kufanya vizuri katika eneo hilo.

Ujio wa Kameta utaifanya Simba kuongeza ushindani katika nafasi hiyo ya beki wa kulia na kumpunguzia majukumu Kapombe.

Inadaiwa kuwa mipango yote ya kumpata beki huyo, imefanywa na Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola ambaye alifanya naye kazi Lipuli, hivyo anaujua ubora wake.

Uongozi wa Simba klabu ya Simba umeshindwa kuweka wazi juu ya usajili wa mchezaji huyo na kusema wachezaji wote wapya watatambulishwa siku iliyopangwa.

Hata hivyo, Kocha Msaidizi wa Lipuli FC, Julio Elieza, aliliambia BINGWA kuwa Simba ilikuwa ikimwinda  mchezaji huyo muda mrefu na kama amesaini halitakuwa jambo geni.

“Kameta ni kati ya wachezaji waliokuwa wanafukuziwa na Simba kwa muda mrefu, kama kuna taarifa za kusaini basi ji jambo la kheru kwa sababu mchezaji ni ngumu mchezaji mzuri kuendelea kuwepo Lipuli itakayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

“Kuna dalili za kuwapoteza wachezaji wote wazuri tuliokuwa nao, hawatakubali kucheza FDL wakati kuna timu za Ligi Kuu zinawahitaji,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -