Tuesday, October 27, 2020

KARAMBO KIPA ANAYESHANGAZA MASHABIKI KUTOITWA TAIFA STARS

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWAMVITA MTANDA


 

MOJA ya nyota wanaofanya vizuri Ligi Kuu Tanzania Bara ni mlinda mlango wa Tanzania Prisons, Aron Karambo, baada ya kuisaidia timu yake hiyo, Prisons msimu uliopita wa Ligi Kuu kumaliza wakiwa nafasi ya nne kutokana na uhodari wake.

Katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipengele cha Mlinda Mlango Bora, Karambo alishika nafasi ya pili akiwa nyuma ya Aishi Manula wa Simba aliyenyakua tuzo hiyo.

Kutokana na ubora wake, ameendelea kuwa gumzo kwa mashabiki wa soka hapa nchini, wakidai kuwa ni kipa ambaye alistahili kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ kutokana na umahiri wake.

Mashabiki hao wanaamini ana uwezo wa kuisaidia timu hiyo ya Taifa Stars ambayo Oktoba 12, mwaka huu itacheza mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) dhidi ya Cape Verde, wakiamini kwamba anaweza kuisaidia timu hiyo kama akipewa nafasi au anaweza kuwa na mchango hapo baadaye kama angeitwa kuwa msaidizi wa Manula kwenye kikosi hicho.

BINGWA lilizungumza na mlinda mlango huyo ambaye anasema alipitia mambo magumu hadi kufikia hatua aliyofikia kwa sasa ya kuweza kuonyesha umahiri wake.

“Namshukuru Mungu kwa kuweza kunifikisha nilipo leo hii, nimepitia mambo mengi magumu, lakini nimeweza kufanikiwa hadi nafahamika,” anasema Karambo.

Akizungumzia mashabiki ambao wamekuwa wakimzungumzia kutokana na ubora wake, Karambo anasema siri ya mafanikio yake ni kitendo cha yeye kuanza kujifunza nafasi hiyo ya mlinda mlango tangu akiwa mdogo kutokana na kuipenda na kugundua kuwa anaimudu.

“Niliipenda sana nafasi ya mlinda mlango na kuamua kupiga tizi tangu nikiwa mdogo, nilipogundua naimudu niliendelea kujifunza zaidi,” anasema Karambo.

“Kitu kingine kilicho nyuma ya mafanikio yangu katika soka yanatokana na utiifu wangu, kuanzia nyumbani kwa wazazi wangu ambao walinisimamia kwa kiasi kikubwa na viongozi wangu wa Tanzania Prisons, akiwamo na Kocha Mkuu, Abdallah Mohamed Bares.”

Karambo anasema alianza kucheza nafasi hiyo tangu akiwa shule ya msingi, ambapo alikuwa anafurahia sana akiona kipa anavyodaka mipira, hali ambayo ilimvuta na kuanza kujaribu kama anaweza.

“Jambo hili lilinifanya tulipokuwa na mechi za kirafiki shuleni, nisifurahie kupangwa nafasi nyingine zaidi ya kipa, hapo ndio marafiki  zangu wakaanza kunikubali kuwa kipa ingawa nilikuwa nafanya vizuri katika mechi nyingine,” anasema Karambo.

Kabla ya mlinda mlango huyo kutua Tanzania Prisons alichezea timu nyingi ikiwamo Polisi Dodoma na kusajiliwa na timu hiyo ya Jeshi la Magereza Tanzania yenye maskani yake mjini Mbeya.

“Nimecheza timu mbalimbali, lakini nyingi zikiwa zile za mtaani ambazo ndio zilianza kunipa jina na baadaye kupata nafasi katika timu ya Polisi Dodoma na hapo ndio naweza kusema nilifanya kazi kubwa na kuonekana na Tanzania Prisons,” anasema Karambo.

Akielezea namna gani amejipanga kupambana na kuhakikisha anaisaidia timu yake msimu huu wa Ligi Kuu, Karambo, anasema: “Najua soka si kazi rahisi kama watu wa nje wanavyofikiria, hii ni kazi ngumu sana, lakini kwa kuwa nina malengo mazuri na timu yangu, lazima nijitume kwa bidii sana kuhakikisha naibeba kama msimu uliopita.”

“Ukizingatia ligi ya msimu huu ni ngumu, hivyo inabidi kupambana sana kufikia malengo, uwezo na jitihada zangu ndio mafanikio ya timu yangu.”

Akizungumzia kutowahi kuitwa timu ya taifa, Karambo anasema: “Wachezaji walioitwa ni bora wana uwezo wa kufanya vizuri, pia muda bado upo kama nimekosa mwaka huu hata mwakani naweza kupata nafasi, cha msingi ni kuomba uzima na kuwaombea wenzetu wakafanye vizuri kwa ajili ya taifa kwa ujumla.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -