Thursday, October 22, 2020

KASI YA MASHAMBULIZI BARCA YAMKUNA VALVERDE

Must Read

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

MADRID, Hispania


KOCHA wa Barcelona, Ernesto Valverde, ameeleza kufurahishwa na kasi ya ushambuliaji ya timu yake, baada ya mastraika, Lionel Messi na Luis Suarez, kuwasaidia mabingwa hao wa La Liga kuiadhibu Huesca kwa mabao 8-2.

Katika mchezo huo wa juzi, Messi  na  Suarez kila mmoja aliifungia timu hiyo mabao mawili huku  Ivan Rakitic, Ousmane Dembele na Jordi Alba kila mmoja akizitikisa nyavu na kuifanya  Barca iondoke na ushindi huo ikiwa nyumbani katika dimba la Camp Nou.

Kabla ya kupata mvua hiyo ya mabao, Barca waliruhusu bao dakika tatu za mwanzo, lakini vinara hao wa soka Hispania wakaweza kupata matatu kabla ya timu hizo kwenda mapumziko jambo ambalo lilimkuna Valverde na akasema kwamba anavyofikiri kikosi chake kingeweza kufunga mengi zaidi.

“Tumefanya mashambulizi mengi, tumecheza vizuri na tumetengeneza nafasi nyingi. Leo ilikuwa ni siku nzuri kwetu, lakini Huesca nao walikuwa na ushindani mkali,” Valverde aliwaambia waandishi wa habari.

“Walikuwa wazuri katika ushambuliaji  kupitia kwa mastaa wao, Juan Camilo  Hernandez ama Alex Gallar. Kuna wakati mechi ilikuwa ngumu lakini tukawa na subira kiasi cha kutosha. Tuliweza kuwadhibiti na tulikuwa na nguvu za kutosha kuweza kutoka nyuma  na kuweza kufunga mabao mengi,” aliongeza kocha huyo.

“Katika kipindi cha kwanza tuliweza kuruhusu bao, la pili nalo hatukulitarajia kwa sababu tulishafunga matatu. Hivyo kipindi cha pili tulibadilika na kuweza kuibadili mechi na kufunga mabao mengi kwa sababu tulicheza vizuri,” alikwenda mbali zaidi kocha huyo.

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote tatu katika mechi za Ligi...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -