Sunday, January 17, 2021

KASI YA OKWI YAWATISHA WANAJESHI

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA WINFRIDA MTOI

UCHEZAJI wa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, umeonekana kuwatisha wengi, kikiwamo kikosi cha timu inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa, Ruvu Shooting.

 

Hivi karibuni Okwi alifanya mambo makubwa akiwa na timu yake ya Taifa ya Uganda, alipoifungia bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Misri, kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018, zitakazofanyika nchini Urusi.

Bao hilo la Okwi limekuja ikiwa ni siku chache baada ya kuisambaratisha Ruvu Shooting kwa kufunga mabao manne peke yake katika ushindi wa mabao 7-0 wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa Agosti 26, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akithibitisha jinsi Okwi anavyowatia tumbo joto wengi alipozungumza na BINGWA jana, mashambuliaji wa Ruvu Shooting, aliyeibuka mfungaji bora msimu uliopita wa ligi, Abdulrahman Mussa, alisema kasi aliyokuja nayo  Mganda huyo inawatisha mno.

Alisema kuwa, kitendo cha Okwi kufunga mabao manne kwenye mechi moja kinamtia presha katika harakati za kutetea kiatu chake cha dhahabu.

Msimu uliopita, Mussa aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara, baada ya kumaliza akiwa na mabao 14, sawa na winga wa zamani wa Yanga, Simon Msuva, anayekipiga katika klabu ya Difaa El Jadid  ya Morocco.

Mussa, aliyerejea nchini jana akitokea Burundi kwenye mashindano ya majeshi kwa nchi wanachama wa ukanda wa Afrika Mashariki, alisema atakosa mchezo wa pili wa ligi wakati timu yake ya Ruvu Shooting itakapovaana na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, kesho.

Alisema licha ya kwamba hata msimu uliopita alikosa mechi mbili za mwanzo, lakini mabao ya Okwi ndiyo yanampa presha katika harakati zake za kutetea tuzo yake ya ufungaji.

“Unapokuwa mfungaji bora halafu akatokea mtu akafunga mabao mengi katika mechi moja kuliko wewe, lazima ujisikie vibaya na kuwa na presha, hata Ronaldo (Cristiano) akisikia Messi (Lionel) kafunga mabao mengi, hawezi akawa katika hali ya kawaida, kwasababu anahitaji kuendelea kuwa bora,” alisema Mussa.

Hata hivyo, alisema bado ana nafasi ya kumfikia Okwi na ataanza kukomaa naye katika mechi ijayo na kuhakikisha jina lake linarudi kwenye orodha ya wafungaji.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -