Saturday, October 31, 2020

KASORO NDOGO ZISITUONDOLEE UTANZANIA WETU

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

WAKATI timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, inatarajia kushuka dimbani leo kuvaana na timu ya Uganda ‘The Cranes’, katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Cameroon, Watanzania wanaonekana kugawanyika katika suala la uzalendo.

Uzalendo ni ile hali ya kupenda kilicho chako, kujitoa au kukitetea kitu kinachokuhusu na kuweka masilahi yako kando, unaweza hata kupoteza uhai kwa ajili ya chako.

Taifa Stars inawakilisha nchi katika michuano hiyo na inacheza ugenini katika Uwanja wa Mandela Namboole.

Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike, aliita wachezaji kambini kujiandaa na mchezo huo, lakini kutokana na taarifa kugongana baadhi wa wachezaji hasa wa Simba walichelewa kuingia katika kambi hiyo Hoteli ya Sea Scape Dar es Salaam.

Amunike alichukua hatua ya kuwaondoa wachezaji hao katika kikosi ambao ni Erasto Nyoni, John Bocco, Shiza Kichuya, Shomari Kapombe, Hassan Dilunga, Jonas Mkude na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Yanga.

Lakini baada ya siku chache kupita, Amunike alitoa msamaha kwa wachezaji hao, akiahidi kuwaita wakati mwingine katika kikosi hicho, kwani nafasi zao zilijazwa na wachezaji wengine aliowaita.

Jambo hilo lilileta mtafaruku mkubwa na kuwagawa wadau wa michezo, wapo waliounga mkono suala hilo na wapo waliopinga vikali hadi kufikia kusema maneno makali.

Baadhi ya mashabiki, wamejipanga kutokuisapoti Stars kwa kuonyesha jinsi walivyokerwa na kitendo cha wachezaji hao kuondolewa katika timu.

Sisi BINGWA tunasema Watanzania tuna kila sababu ya kuisapoti timu yetu, iweze kufanya vema Uganda, kwani sisi  tuna nafasi ya kuleta mafanikio katika timu.

Hizi kasoro ndogo zilizojitokeza zisituondolee Utanzania wetu, shime Watanzania twende tukaishangilie Stars yetu.

Katika akili za kawaida hata wapinzani wetu Uganda wakiyasikia haya watatucheka, kwani mara zote wamekua wakituona tukiwa watu wenye umoja na mshikamano kwa timu yetu.

Tusiiache Taifa Stars kama yatima, tuungane kwa pamoja kama Taifa na kuishangilia kwa nguvu na tuachane na mambo ya kuhatarisha umoja na mshikamano wetu.

Watanzania ni watu waelewa wenye ukarimu, acha tutofautiane katika masuala mengine lakini si hili la utaifa wetu.

Tumekua mashahidi mwaka huu wakati wa michuano ya Kombe la Dunia, iliyofanyika nchini Urusi Juni 14 hadi Julai, jinsi mashabiki wa mataifa yaliyoshiriki walivyoungana na kusapoti timu zao.

Mashabiki wale si kwamba hawana tofauti nchini mwao, lakini walizisahau na kuungana pamoja kwa ajili ya kushangilia timu zao.

BINGWA tunaamini hatutaponzwa na kasoro zilizojitokeza, bali tutaungana katika suala hili la kitaifa na kuishangilia Taifa Stars.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -