Wednesday, October 28, 2020

KATIBU MPYA YANGA ASHTUKA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

*Amtoa nishai Nyika alipomwomba fedha za kambi

*Asema hayupo tayari kwenda jela kisa fedha za Yanga

HUSSEIN OMARI NA MICHAEL MAURUS

KAIMU Katibu Mkuu wa Yanga, Omari Kaaya, amedaiwa kuonyesha ujasiri wa hali ya juu baada ya kumgomea Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Hussein Nyika, kumpa fedha za kulipia kambi ya timu hiyo iliyowekwa Morogoro katika Hoteli ya Kings Way.

Habari kutoka ndani ya Yanga, zinadai kuwa Nyika alifika katika ofisi za klabu hiyo zilizopo katika makutano ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam akimtaka Kaaya ampe shilingi 31,840,000 ili kulipia kambi.

Mtoa habari wetu huyo alidai kuwa alimgomea Nyika akihoji matumizi ya fedha walizoingiza kupitia mechi tatu za kirafiki ambazo timu yao ilicheza mkoani Morogoro.

“Nyika alipeleka bili ya kambi waliyokaa Morogoro, baada ya Omari kuipokea, akahoji yalipo mapato ya mechi za kirafiki walizocheza huko Moro, hapo ndipo vurugu zilipoanza na kutupiana maneno makali,” alidai mtoa habari wetu huyo.

Chanzo chetu hicho kilisisitiza kuwa kabla ya Yanga kwenda kuweka kambi Morogoro, Kaaya alishauri timu ikae Dar es Salaam kwani walishakubaliana na Azam Media timu icheze mechi tatu za kirafiki zionyeshwe na Azam TV na klabu kupewa shilingi milioni 10 kila mchezo, lakini akina Nyika wakakataa.

Alidai kuwa pamoja na fedha hizo, Yanga pia ingenufaika na mapato ya viingilio kwa kugawana na timu ambayo wangecheza nayo.

BINGWA lilimtafuta Nyika ili kuthibitisha madai hayo, lakini alipopigiwa simu na mwandishi wetu, hakuweza kutoa maelezo yoyote zaidi ya kuishia kuuliza: “Unasemaje? Unasemaje? Unasemaje?…”

Gazeti hili lilimtafuta Kaaya kuthibitisha madai hayo ambapo naye alikanusha kutokea tukio hilo akisisitiza kama kuna masuala yoyote ya fedha, Nyika angeenda kwa mhasibu na si kwake kwani yeye ni mwidhinishaji tu.

“Hakuna kitu kama hicho, huo ni uzushi tu unaopikwa na watu. Kwanza timu bado ipo kambini Morogoro inaondoka kesho (leo) kuja Dar es Salaam hivyo kama ni malipo ya hoteli, kesho ndio itajulikana.

“Kama ni kudaiwa, hiyo si kitu kipya, klabu imekuwa na madeni ya muda mrefu hata Mkwassa (Charles-Katibu wa Yanga aliyejiuzulu), aliyakuta na kuyaacha. Huu si wakati wa kubomoa, ni wakati wa kujenga kwa kuandika mema ya klabu, kuhamasisha mashabiki kuwa karibu na timu yao.

“Keshokutwa (kesho) tunacheza na Waarabu (USM Alger ya Algeria), mnatakiwa kuwahamasisha mashabiki kuja kwa wingi uwanjani waione timu yao na si hizo habari za uchochezi,” alisisitiza Kaaya.

Kitendo cha Kaaya kukanusha habari hiyo, kililishtua BINGWA na kuamua kuchimba zaidi ambapo lilimtafuta mmoja wa wanachama wa muda mrefu aliyeanza kuitumikia Yanga tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990 ambaye alitoboa kila kitu.

“Nyie BINGWA kiboko, hadi hiyo mmeinasa…ni kweli hilo tukio limetokea klabuni Kaaya anaficha tu kwa kuwa Nyika ni jamaa yake na ndiye aliyechangia kumfikisha katika nafasi ya ukatibu.

“Ni kweli kabisa waligombana baada ya katibu kuombwa fedha za kulipia kambi ya Morogoro ndipo naye alipoomba mrejesho wa mapato ya mechi za kirafiki walizocheza Morogoro. Vijana wa ‘task force’ ndio waliowatuliza la sivyo wangeshikana mashati.

“Walimweka (Kaaya) wakijua ni mtu wao hivyo wangemtumia watakavyo, lakini amewageuka. Jamaa (Kaaya) anaonekana kuhofia yasije kumkuta kama yaliyowakuta viongozi wa Simba waliopo mahabusu kwa tuhuma za utakatishaji wa fedha,” alidai mtoa habari wetu huyo.

Alisema kuwa mbali ya tukio hilo, jana kulikuwa na kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kujadili juu ya hatima yao kwani muda wao wa kuwapo madarakani umekwisha.

“Kwa kawaida kamati ile inatakiwa kuongezewa muda kila baada ya miaka miwili, lakini kwa kuwa hakuna uongozi, hilo halikufanyika, hivyo kuna uwezekano mkubwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) ikasimamia uchaguzi wetu,” alidokeza.

BINGWA lilijichimbia mjini Morogoro kwa wiki mbili kufuatilia mazoezi ya Yanga, liliwasiliana na uongozi wa Hoteli ya Kings Way kufahamu deni wanaloidai Yanga na kupewa kila kitu.

“Hadi leo (jana), tunaidai Yanga shilingi 33,832,000,” alisema mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo ‘bab kubwa’ iliyopo eneo la Msamvu, karibu na stendi kuu ya mabasi mjini Morogoro.

Juu ya fedha walizolipwa hadi jana mchana na klabu hiyo, alisema kuwa siku ya kwanza walilipwa shilingi milioni 5.5 kabla ya baadaye kupewa shilingi 600,000.

Kuhusiana na fedha walizovuna Yanga, kupitia mechi za kirafiki walizocheza Morogoro, dhidi ya Mawenzi Market kwenye Uwanja wa Jamhuri, inadaiwa walilipwa shilingi milioni 15, huku wengine wakidai ni shilingi milioni 12.

Mechi hiyo ilinunuliwa na mmoja wa wadau wa soka mkoani humo kama ilivyokuwa kwa ile waliyocheza na Kilosa Kombaini Uwanja wa CCM Azimio na Wanajangwani hao kulipwa shilingi milioni 6 kama BINGWA lilivyotonywa jana na mmoja wa viongozi waliokuwa karibu na timu mkoani humo.

“Kwa upande wa mchezo tuliocheza na Mkamba Rangers, klabu ilipata mgao wa shilingi milioni saba na ushee kwani fedha zilizopatikana ni shilingi milioni 11 hivyo wenyeji walichukua milioni tatu na pointi kadhaa,” alisema mtoa habari wetu wa uhakika kutoka Morogoro.

Alisema kuwa waandaaji wa mchezo huo na Mkamba Rangers wa Kilombero, walikuwa tayari kuipa Yanga 70% ya mapato ya viingilio huku wao wakibakiwa na 30% ambazo zingegharamia maandalizi yote ya mchezo huo kwani lengo lao halikuwa faida bali kuwapa uhondo mashabiki wa soka wa eneo lao hilo.

Baada ya kujifua kwa wiki mbili Morogoro, kikosi cha Yanga kinatua Dar es Salaam leo tayari kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya USM Alger kwenye Uwanja wa Taifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -