Friday, December 4, 2020

KAZE YUPO KAZINI:Atwaa pointi tatu mfululizo Yanga ikiichapa KMC 2-1 CCM Kirumba,Amwagia sifa Waziri Jr, atamba kuendeleza vichapo Ligi Kuu Bara

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA MWANDISHI WETU, MWANZA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amethibitisha kuwa yupo kazini baada ya jana kukiongoza kikosi chake kupata ushindi wake wa mabao 2-1 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini hapa.

Ushindi huo, umeiwezesha Yanga kuzidi kujikita katika nafasi ya pili ya ligi hiyo, baada ya kufikisha pointi 19 kutokana na mechi saba, ikiwa nyumba ya Azam iliyopo kileleni na alama 21, Wanalambalamba hao nao wakiwa wamecheza michezo saba.

Alikuwa ni Waziri Junior aliyeifungia Yanga bao la pili la ushindi dakika ya 61 baada ya timu hizo kuwa sare ya bao 1-1, KMC wakianza kutikisa nyavu kupitia kwa Hassan Kabunda dakika ya 27, kabla ya Tuisila Kisinda kusawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 41.

Kwa upande mwingine, ushindi wa jana wa Yanga, umezidi kutoa picha halisi ya Kaze kuwa ni mtu wa kazi asiyejali jina la mchezaji zaidi ya uwezo wake uwanjani.

Hilo limethibitishwa na uamuzi wake wa kumwanzisha Junior ambaye hakuwa akianza kikosi cha kwanza kabla ya ujio wa Kaze na mwisho wa siku, mshambuliaji huyo akaipa timu yake bao la ushindi.

Mbali ya Junior, kwa mara nyingine, Kaze alimpa nafasi Farid Mussa ambaye alitokea benchi na kuchonga kona iliyozaa bao la kichwa lililofungwa na Farid.

Mchezaji mwingine mpya katika kikosi kilichocheza jana wa Yanga, alikuwa ni beki wa kati, Shaibu Abdallah ‘Ninja’ ambaye hakuwa akipewa nafasi na Mserbia   Zlatko Krmpostic aliyetimuliwa.

Akimzungumzia Junior, Kaze alisema kuwa alimpa nafasi kutokana na juhudi zake mazoezini na amefurahi kuona mchezaji huyo ameiwezesha timu yake kupata pointi tatu muhimu.

Alisema alianza kuvutiwa na uchezaji wa Junior mazoezini, hasa uwezo wake wa kushuka chini kuchukua mipira, akiamini anamudu kucheza nyuma ya mshambuliaji wa mbele kama alivyofanya jana.

Ushindi wa jana wa Yanga ni wa pili mfululizo tangu Kaze alipopewa mikoba ya kukinoa kikosi hicho akichukua nafasi ya Krmpostic, wa kwanza ukiwa ni ule dhidi ya Polisi Tanzania walioshinda bao 1-0 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Alhamisi ya wiki iliyopita.

Kwa ujumla, mchezo wa jana baina ya Yanga na KMC, ulikuwa ni mkali na wa kuvutia, huku timu zote mbili zikicheza soka la kufunguka.

Hata hivyo, wenyeji KMC ndio walioonekana kutawala zaidi, wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara, lakini ngome ya Yanga chini ya mabeki, Lamine Moro na Bakari Mwamnyeto, ilikuwa imara kuondosha hatari kadhaa zilizoelekezwa langoni mwao.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Ramadhan Kayoko kutoka jijini Dar es Salaam, walikuwa ni KMC walioanza kulifikia lango la Yanga na kupata kona dakika ya pili ambayo haikuzaa matunda.

Dakika ya tatu, Deus Kaseke wa Yanga, alipiga faulo iliyotokana na kuchezewa rafu kwa Lamine nje kidogo ya 18, lakini mpira huo wa adhabu haukuweza kuzaa matunda.

Dakika ya 14, beki wa kushoto wa Yanga, Yassin Mustapha, alichonga krosi safi kwenda langoni mwa KMC, lakini beki wa timu hiyo, Andrew Vincent ‘Dante’, aliwahi na kuokoa hatari hiyo.

Dakika ya 15, KMC walifanya shambulizi langoni mwa Yanga ambalo hata hivyo, liliishia kwa mpira kutoka nje.

Yanga walikaribia kupata bao dakika ya 22 baada ya beki wao wa kulia, Kibwana Shomary, kuchonga krosi safi ambayo hata hivyo, ilichelewa kumfikia Junior aliyekuwa ndani ya sita na mpira kutoka nje.

Dakika ya 24, Kisinda alipiga krosi inayomkuta Junior ambaye akiwa ndani ya sita, alipiga mpira kwa kisigino na kutoka nje.

Dakika tatu baada ya shambulizi hilo la Yanga, KMC walijibu mapigo na kupata bao kupitia kwa Kabunda aliyeihadaa ngome ya wapinzani wao hao na kuachia shuti kali lililotinga moja kwa moja nyavuni na kumwacha kipa Metacha Mnata akichupa kuokoa bila mafanikio.

Baada ya kufunga bao hilo, Kabunda alionyeshwa kadi ya njano kwa kosa la kushangilia kwa kuvaa kinyago.

Dakika ya 40, Michael Sarpong alifanyiwa madhambi ndani ya boksi wakati akiwa katika harakati za kupokea mpira wa krosi uliopigwa na Mustapha na mwamuzi kuamuru ipigwe penalti.

Penalti hiyo ilipigwa na Kisinda aliyemchambua kama karanga kipa wa KMC, Juma Kasena na kuukodolea macho mpira ukienda upande wa kulia wa lango, huku yeye akielekea kushoto.

Dakika ya 49, Lamine alionyeshwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Paul Godfrey wa KMC.

Dakika ya 61, Junior aliwainua ‘Wananchi’ vitini baada ya kuifungia Yanga bao la pili kwa kichwa, akipokea mpira wa kona uliopigwa na Faridi.

Baada ya kufunga bao hilo, naye alionyeshwa kadi ya njano kutokana na kitendo cha kuvua jezi wakati akishangilia kuonyesha maneno yaliyoandikwa katika fulana yake ya ndani ‘King of CCM Kirumba’, yaani yeye ni Mfalme wa Uwanja wa CCM Kirumba.

Pamoja na mashambulizi ya pande zote mbili, bao hilo la Junior, liliduma hadi dakika ya mwisho na kuishuhudia Yanga ikiondoka na pointi zote tatu.

KMC: Juma Kaseja, Israel Mwenda, David Brayson, Lusajo Mwaikenda, Andrew Vincent ‘Dante’, Jeans Baptiste, Abdul Hillary/Martin Kigi (dak72), Kenny Ally, Paul Peter, Emmanuel Mvuyekule na Hassan Kabunda.

YANGA: Metacha Mnata, Shomary Kibwana, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda/Andallah Shaibu (dk 88), Feisal Salum ‘Fei Toto’, Deus Kaseke/Farid Mussa (dk 59), Waziri Junior/Haruna Niyonzima, Michael Sarpong.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -