Sunday, November 29, 2020

KENNY ALLY ZAO LA COPA- COCA COLA LINALOTESA NA MBEYA CITY

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

MAISHA ya mwanadamu ni safari ndefu inayohitaji uvumilivu wa kiwango cha hali ya juu.

Nasema ni safari ndefu kwakua katika maisha kuna changamoto mbali mbali ambazo tumekuwa tukikutana nazo.

Wapo ambao wamekuwa wakitumia changamoto hizo kama kichocheo cha kuwafanya wasonge mbele, pia wapo  wanaokata tamaa na kurudi nyuma.

Watu wengi ambao leo hii tunawaweka katika kundi la waliofanikiwa katika maisha, wakikusimulia historia zao utasikia walikutana na changamoto mbali mbali ambazo kama wasingesimama vema wangekata tamaa na kurudi nyuma.

Maisha ndivyo yalivyo, yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu na kujituma katika kile unachoamini kinaweza kukupa mafanikio.

Kiungo mahiri wa Mbeya City, KennyAlly, kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji mahiri wa Ligi Kuu Tanzania Bara hususani wanaocheza katika eneo la kiungo ambaye licha ya changamoto tulizonazo katika soka la hapa nyumbani Tanzania amekuwa akipambana na kusonga mbele.

Ally kabla ya kufika hapa baadhi ya klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara zilimtolea udenda zikitamani kumsajili, amepitia changamoto mbali mbali katika maisha yake ya soka.

Kiungo huyu mzaliwa wa mkoani Mbeya alianza kucheza soka tangu akiwa kijana mdogo akichezea timu za mtaani.

Lakini ndoto zake za kutaka kuwa staa wa soka zilianza kutimia pale aliposhiriki michuano maalumu ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 ya Copa Coca-Cola mwaka 2008 nchini Brazil.

Katika mashindano hayo Tanzania ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kuzifunga timu ya Argertina (2-0), Peru (5-1) na kutoka sare na Chile (0-0).

Ilifuzu nusu fainali ambako iliibwaga Paraguay kwa kuichapa mabao 3-1 kisha ikatinga fainali na kukutana na Chile kwa mara nyingine na kuichapa bao 1-0.

Wachezaji wengine waliokuwamo kwenye kikosi cha Serengeti ni Kabari Faraji, Mohamed Hussein, Ahmed Mohamed Chimpele, Sadik Gwaza, Adili Adam, Himid Mao na Faraji Hamad.

Wengine ni Lambele Jerome, Karim Sule, Zahoro Ismail, Jukumu Kibanda, Dotto John, Joseph Mahundi, Hemed Suleiman.

Pamoja na kikosi hicho kuonekana kimesheheni wachezaji wenye vipaji, ni wachache tu ndiyo walioendeleza moto kwa kupiga hatua nyingine mbele kwa kusajiliwa na klabu mbali mbali za ndani na nje ya nchi na miongoni mwao ni Ali ambaye anatamba na Mbeya City.

Yanga ni miongoni mwa klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara zinazodaiwa zimekuwa zikimfuatilia kiungo huyo kwa muda mrefu zikitaka kumsajili.

Almanusura Yanga imsajili katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo la msimu uliopita, lakini dili hilo halikufanikiwa baada ya pande hizo mbili kutoafikiana katika suala zima la kiwango cha fedha.

Ifahamike kwamba kwa muda mrefu Yanga imekuwa na tatizo la kukosa kiungo makini wa ukabaji tangu ilipoachana na Athuman Iddi ‘Chuji’.

Kiungo huyo ndiye aliyeifunga Yanga bao la pili kwa mkwaju wa mpira wa adhabu katika  pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara  mzunguko wa kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya ambapo Mbeya City ilishinda mabao 2-1.

Hata hivyo, bao hilo lilipingwa na wachezaji wa Yanga ambao walidai mpira ulipigwa kabla ya mwamuzi kupiga filimbi ya kuashiria kuruhusu upigwe, ingawa baada ya mwamuzi wa kati kujadiliana na wasaidizi wake hatimaye lilikubaliwa.

Ni wazi kama Yanga ingefanikiwa kunasa saini ya Ally ingeweza kupata suluhisho la tatizo la kiungo mkabaji ambalo limekuwa sugu kwa msimu kadhaa sasa tangu kuondoka kwa Chuji.

Hata katika mchezo wa mzunguko wa pili dhidi ya Simba uliofanyika hivi karibuni na matokeo kuwa sare ya mabao 2-2, Ally alionyesha kiwango cha juu ambapo alifanikiwa kukata mawasiliano na kiungo wa Simba.

Bao lake alilowafunga Wekundu wa Msimbazi lilitosha kuthibitisha ni kiungo wa kiwango cha juu mwenye uwezo pia wa kufunga mabao.

Bao hilo lilikuwa hivi, Ally alipokea mpira akamchomekea pasi mchezaji mwenzake Ditram Nchimbi, ambaye alipiga krosi iliyomkuta Ally ambaye aliukwamisha mpira wavuni hakika lilikuwa bao la kuvutia.

Kuhusu Copa-Coca Cola

Michuano hii yenye lengo la kuinua vipaji kwa Tanzania ilianza rasmi mwaka 2007, mpaka sasa imeibua nyota wengi ambao wanatamba katika klabu mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Mara ya mwisho michuano hii ilifanyika  mwaka 2014, ambapo timu ya Mkoa wa Dodoma ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -