Tuesday, November 24, 2020

KENYA WAIHOFIA TANZANIA MBIO ZA NYIKA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA WINFRIDA MTOI

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday, amedai Kenya wameanza kuihofia Tanzania kuelekea mashindano ya mbio za nyika za dunia zitakazoanza Machi 26 hadi Aprili mosi, mwaka huu nchini Uganda.

Gidabuday alisema hali hiyo inatokana na rekodi ya wanariadha wa Tanzania katika michuano waliyoshiriki hivi karibuni ikiwamo mashindano ya Taifa.

Alisema tangu michuano ya mbio za nyika imeanza, Kenya na Ethiopia ndio walikuwa wanapokezana ubingwa mara nyingi kuliko nchi nyingine.

Gidabuday alisema ushiriki wa Tanzania unawatia hofu hasa ukizingatia michuano hiyo inafanyika Afrika Mashariki.

“Kenya wanatuhofia katika mashindano hayo kwa sababu siku tuliyofanya michuano ya kuchagua timu ya Taifa, ndiyo siku Kenya pia walifanya mashindano ya Taifa na bingwa wao hajamfikia bingwa wetu, Emmanuel Giniki,” alisema.

Alisema kikosi wanachopeleka ni kikubwa kuliko kilichoshiriki michuano hiyo mwaka 2015 nchini China na kushika nafasi ya sita.

“Watanzania watarajie makubwa kwenye mashindano haya kwa kuwa tulijipanga tangu mwaka jana Desemba, ukizingatia tunapeleka kikosi kikubwa ambapo kila mbio tutakuwepo,” alisema Gidabuday.

Alisema uzuri wa michuano hiyo, mshindi wa kwanza hadi wa sita anapata zawadi kuanzia dola za Kimarekani 6,000.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -