Friday, October 23, 2020

KESSY ATAANZAJE KUMWEKA BENCHI ABDUL?

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA ONESMO KAPINGA

PAMOJA na beki, Hassan Ramadhan ‘Kessy’, kuitikisa Simba alipoamua kujiunga na Yanga katika dirisha dogo la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), baada ya timu hiyo kutinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho, lakini kwa sasa anaonekana ni mchezaji wa kawaida sana.

Uondokaji wa Kessy katika klabu ya Simba ulikuwa wa mbwembwe akijua anakoenda ataishi maisha ya peponi, lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele sidhani kama atakuwa na maisha aliyofikiria akiwa huko.

Mbwembwe alizoonesha Kessy kwa mwajiri wake wa zamani, Simba zilionekana kuwaudhi kwa namna moja au nyingine, hali iliyowafanya waanze kula naye sahani moja kwa kumwekea kauzibe.

Kutokana na jeuri zake, Simba walimwekea kauzibe ili asicheze mechi za Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kuanza kuitumikia Yanga akiwa ana mkataba na klabu yake ya zamani.

Uamuzi wake wa kusaini Yanga ulikuwa sahihi baada ya kubakisha mkataba wake wa miezi sita Simba, lakini kitendo cha kuanza kufanya kazi kwa karibu na Wanajangwani hao, hapo ndipo alipofanya kosa.

Kitendo hicho kilionekana kumgharimu kwani mbwembwe zake ziliishia sakafuni, kwani hakuweza kuingia Yanga kwa asimilia 100 katika michuano ya Kombe la Shirikisho kutokana na sakata lake.

Kwa kifupi, usajili wa Kessy ulikwama CAF baada ya kuonekana alikuwa bado ni mchezaji wa Simba na kusubiri hadi dirisha la usajili la Ligi Kuu Tanzania Bara lilipofunguliwa.

Lakini Simba waliendelea kukomaa na beki huyo kwa madai alivunja mkataba na hatimaye Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF ilitoa uamuzi wake wakuitaka Yanga iilipe Simba.

Uondokaji wa Kessy kwa kiasi fulani uliwaumiza mashabiki wa Simba, kutokana na alikuwa ni mchezaji mzuri katika kikosi chao.

Pengine mashabiki wa Simba waliumia mara mbili, mosi aliondoka huku wakiwa bado wanamhitaji katika kikosi chao, lakini kitendo la kwenda kujiunga na wapinzani nacho kilichangia kwa kiasi kikubwa.

Kwa kuwa ulikuwa ni uamuzi wake binafsi hakuna mtu ambaye aliweza kumshauri aendelee kubaki Simba, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuingilia nafsi yake.

Ilikuwa piga, ua, Kessy lazima aanze katika kikosi cha kwanza cha Simba, kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Ramadhan Singano, aliyejiunga na Azam msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.

Maisha yake aliyokuwa akiishi Simba si anayoisha kwa sasa Yanga, kwani ameanza kusugua benchi kama wachezaji wengine waliosajiliwa kutoka timu nyingine.

Kessy amefikia kwenye benchi lile lile la Yanga walilofikia akina Said Bahanuzi, Malimi Busungu, Hussein Javu na wengineo na baadaye walifikia kutengeneza mitindo ya kusuka nywele.

Sitaona ajabu Kessy akimaliza mkataba wake wa miaka miwili Yanga akiwa kama mwenzake Busungu ambaye hana namba katika kikosi hicho.

Inanipa wasiwasi kama Kessy ataweza kupata namba kwa beki anayepanda na kushuka kwa spidi kali, Abdul Juma, labda ajitahidi sana.

Kwa kiwango alichokionesha Abdul katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo, naamini uwezo wake uko juu na Kessy atasubiri sana kuanza katika kikosi hicho.

Kwa hali inavyoonekana, tayari kocha mpya wa timu hiyo, George Lwandamina, atakuwa amepata kikosi chake cha kwanza na Kessy ameshindwa kumshawishi ili aweze kupata namba ya kudumu.

Inatarajia kama Abdul anamfanyia kazi nzuri kocha wake Lwandamina, nafasi ya Kessy itakuwepo? Atasubiri kwenye lile benchi la akina Busungu.

Mzee wa Kupasua anaona kwamba, Kessy hakuchanga vizuri karata zake, kwani alitakiwa kujua pale Yanga kuna beki anaitwa Abdul Juma, ambaye ana kiwango zaidi yake.

Lakini aliona fahari kwenda kujiunga na Yanga ambako benchi linamhusu sana tena sana.

Kessy ataanzaje kumweka benchi Abdul kutokana na kiwango anachoendelea kuonyesha ligi kuu na michuano ya kimataifa?.

kapssmo@gmail.com 0716985381

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -