Wednesday, October 21, 2020

KIBA ATAKA UBINGWA COASTAL UNION

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA OSCAR ASSENGA, TANGA


STRAIKA wa timu ya Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’, Ali Kiba, amesema anatamani kuona timu hiyo ikitwaa ubingwa kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwani hilo linawezekana.

Kiba aliyasema hayo juzi mara baada ya kumalizika kwa mechi yao dhidi ya KMC, ambapo timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1, mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga.

Katika mchezo huo, straika huyo aliingia kipindi cha pili ambapo alikwenda moja kwa moja jukwaa ambalo walikuwa wamekaa viongozi wa timu hiyo, akikitazama kikosi cha timu hiyo ndani ya dakika 45 za kipindi cha pili.

Alisema hivi sasa ligi hiyo ndio kwanza imeanza na  kuchezwa mechi chache, hivyo nafasi ya timu hiyo kutwaa ubingwa bado ipo huku akiahidi atashirikiana na wachezaji wengine waliopo kufanikisha azma hiyo.

“Sikuonekana uwanjani muda kwa sababu nilikuwa safarini, sifikirii kama kuwa nje ya kikosi kunaweza kuniathiri, ninachokifikiria sasa ni kujiunga pamoja na wachezaji wenzangu, kutengeneza umoja ambao utakuwa na tija,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -