Tuesday, January 19, 2021

KIPA KIBOKO YA BRAZIL AFUZU SIMBA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAITUNI KIBWANA


YULE kipa kiboko ya Wabrazil, Daniel Agyei, amefuzu vipimo kwa ajili ya kuijunga na Simba katika usajili wa dirisha dogo, unaotarajiwa kufungwa Desemba 15, mwaka huu.

Agyei ni kipa nyota ambaye Wabrazil hawatomsahau baada ya kuwahenyesha kwa kuokoa michomo yao ndani ya dakika 120 na kisha kuangua panalti mbili katika fainali ya Kombe la Dunia la Vijana chini ya miaka 20 mwaka 2009.

Katika mechi hiyo ambayo Ghana walishinda mabao 4-3 kwa mikwaji ya penalty, Agyei alipangua penalti ya tatu na ya sita na kisha kuipa Ghana Ubingwa huo.

Akizungumza na BINGWA, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji  ya Simba, Said Tully, alithibitisha kufanyiwa vipimo kwa kipa huyo  na kwamba jana alitarajiwa pia kupewa mkataba rasmi wa kujiunga na Simba.

“Tumempima kwa sababu yule ni binadamu, lolote linaweza kutokea alafu kama atakuwa mgonjwa ataweza vipi kukumbana na mikikimikiki ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Amefuzu vipimo na huenda leo jioni (jana jioni) akasaini mkataba,” alisema.

Alipotakiwa kutaja nyota atakayekatwa kwenye kikosi hicho, Tully alisema kuwa kazi hiyo ni ya Kamati ya Usajili chini ya Mwenyeki wake, Zacharia Hans Pope.

Licha ya kutotaja, BINGWA inatambua nyota Mussa Ndusha ambaye hajapata nafasi mzunguko wa kwanza na beki Besala Bukungu, hawapo salama kwenye kikosi hicho kwa sasa.

Ujio wa Agyei unazidisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni kwenye kikosi hicho ambacho tayari idadi hiyo walishaitimiza, hivyo lazima akatwe mmoja ili kumpisha kipa huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -