Wednesday, October 28, 2020

Kiboko ya Kichuya huyoo Yanga

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR,

NYOTA watatu wa Simba, kamwe hawatamsahau beki wa Mbao FC, Asante Kwasi, kutokana na umahiri aliouonyesha beki huyo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Tayari beki huyo ameelezea shauku yake ya kukipiga Yanga akiamini anao uwezo wa kupata namba ndani ya kikosi hicho cha Jangwani.

Katika mchezo wao na Simba juzi, nyota hatari wa Wekundu wa Msimbazi hao kama winga Shiza Kichuya, Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo, walijikuta wakiambulia patupu baada ya kudhibitiwa vilivyo na Kwasi.

Kichuya ambaye mashabiki wa Yanga hawamsahau tangu afunge bao la kusawazisha baada ya kona aliyoipiga kwenda moja kwa moja nyavuni  dakika ya 87, lakini pia akiwa ndiye kinara wa ufungaji mabao Ligi Kuu Bara, akiwa amecheka na nyavu mara saba, juzi alishindwa kufurukuta mbele ya beki huyo wa Mbao.

Akizungumza na BINGWA, Kwasi alisema bado ana safari ndefu ya mafanikio katika soka ndio maana amekuwa akicheza kwa kujituma zaidi uwanjani na kuwadhibiti vilivyo washambuliaji hatari kadiri anavyotaka.

“Simba ni timu kubwa, unapocheza na timu kama hii kuna mambo mengi ndani hasa kwa sisi wachezaji ambao tunacheza kwenye timu zenye majina madogo hivyo ni lazima tujitume tuweze kujitangaza zaidi katika soko,” alisema Kwasi.

Kwasi ambaye amejiunga na Mbao FC akitokea Mbambane ya nchini Swaziland, alisisitiza kuwa amekuja nchini kufanya kazi na moja ya ndoto yake ni kucheza katika timu hizo mbili kubwa hapa nchini, zaidi ikiwa ni Yanga japo pia iwapo Simba watamtaka atakuwa tayari kujiunga nao.

Katika mchezo huo wa juzi, Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Muzamiru Yasin na hivyo kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa VPL kwa kufikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 10, wakifuatiwa na Stand United yenye pointi 20.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -