Monday, November 23, 2020

Kichuya aamsha hisia mpya Simba

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA,

KITENDO cha winga wa Simba, Shiza Kichuya, kwenda kushangilia bao alilofunga dhidi ya Azam FC kwenye bango lililokuwa na picha ya Patrick Mafisango, kimeamsha hisia mpya ndani ya klabu hiyo.

Kichuya alifunga bao lililoipa Simba ushindi wa bao 1-0 katika mchezo huo dhidi ya Wanalambalamba hao na kukaa kileleni, mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Baada ya bao hilo, Kichuya alikimbilia kwenye bango hilo lililokuwa na picha ya Mafisango ambaye alikuwa ni mmoja wa kiungo wao mahiri kabisa kuwahi kutokea Msimbazi, kitendo ambacho kilipokewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa Simba na wengine.

Licha ya mashabiki wa Simba kuonekana kushangilia kwa nguvu mno bao hilo, lakini baada ya Kichuya kukimbilia picha hiyo ya Mafisango, baadhi yao walijikuta wakisahau shangwe hizo na kumkumbuka mkali wao huyo aliyefariki maeneo ya Keko kwa ajali ya gari.

“Dah! Jamaa (Kichuya), kanikumbusha mbali sana, yaani katukumbusha jinsi Mafisango alivyokuwa msaada mkubwa kwetu kwa jinsi alivyokuwa akimiliki pale katikati ya uwanja huku akifunga mabao muhimu. Kwa kweli hatutamsahau,” alisema shabiki mmoja huku akisapotiwa na wenzake.

Mjadala huo wa Mafisango uliendelea katika vijiwe mbalimbali hata baada ya mchezo huo, kudhihirisha jinsi kitendo alichokifanya Kichuya kwenda kushangilia bao lake kwenye picha ya mchezaji huyo kilivyowagusa wengi.

Mafisango ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji tegemeo wa Simba, alifariki mwaka 2012, kwa ajali ya gari eneo la Keko, karibu na Chuo cha Veta, jijini Dar es Salaam, baada ya gari alilokuwamo kuacha njia na kugonga mti uliokuwa pembeni ya barabara.

Kiungo huyo ambaye pia alikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga mabao, alizikwa Mei 20 mwaka huo nchini kwao DR Congo katika eneo la Lemba, nje kidogo ya Jiji la Kinshasa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -