Tuesday, November 24, 2020

Kichuya ‘abatizwa’ jina la ‘Mwendo Kasi’

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

GEORGE KAYALA NA MWANI NYANGASA, MBEYA

STRAIKA hatari wa Simba kwa sasa, Shiza Kichuya, amebatizwa jina la ‘Mwendo Kasi’ na mashabiki wa soka mkoani Mbeya kutokana na kasi yake aliyoionyesha kwenye mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu.

Jina hilo alibatizwa rasmi juzi katika mechi kati ya timu yake na Mbeya City iliyofanyika katika Uwanja wa Sokoine ambapo Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-0, huku mchezaji huyo akifunga bao moja baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Wagonga Nyundo hao wa Mbeya.

Akiwa kwenye winga ya kushoto, Kichuya alitanguliziwa pasi safi na kiungo Jonas Mkude na kumzidi mbio beki wa Mbeya City, John Kabanda, kabla ya kukokota mpira na kuachia shuti kali lililojaa moja kwa moja wavuni.

Mashabiki kadhaa wa timu hiyo waliliambia gazeti hili kuwa hakuna ubishi jina hilo linaendana na hali halisi kutokana na anachokifanya ndani ya uwanja.

Mpaka sasa kati ya mabao 6 aliyokwisha ipachikia timu yake matatu yametokana na ujanja wa kuwatoka walinzi wa timu pinzani kwa kutimua mbio na kufunga.

Hali kadhalika kati ya mabao 15 ambayo Simba imeshafunga katika VPL msimu huu, Kichuya ametoa msaada wa mabao saba peke yake yote yakitokana na uwezo wake binafsi wa kukimbia.

Kichuya ambaye amesajiliwa msimu huu akitokea Mtibwa Sugar, ameibuka kuwa kipenzi cha mashabiki na viongozi wa Simba.

Hali hiyo imesababisha Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hanspope, kuahidi kumzawadia gari dogo la kutembelea aina ya Raum.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo uliokuwepo mjini hapa, zimesema kuwa Hanspope anatarajiwa kumkabidhi Kichuya gari hilo Jumatatu ijayo.

Hiyo itakuwa ni mara ya pili kiongozi huyo kumzawadia gari mchezaji msimu huu kutokana na kufanya vizuri ndani ya timu hiyo.

Mwezi uliopita mchezaji mwingine, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, alizawadiwa gari aina ya Raum lenye thamani ya shilingi milioni 12.

Kwa upande wake staa huyo ameliambia BINGWA kuwa akili yake yote ipo kwenye kuhakikisha anaipa ubingwa wa ligi kuu klabu yake ya Simba na katu hafikirii kuhusu kuibuka mfungaji bora kwa sababu kwake yeye timu kwanza mengine baadaye.

Akizungumza na BINGWA jana, Kichuya mwenye mabao sita katika msimamo wa wafungaji akiwa anafuatiwa na Amissi Tambwe wa Yanga mwenye mabao manne, alisema utimilifu wa furaha yake ni kuona Simba inashiriki mashindano ya kimataifa mwakani.

“Sikuja Simba kuuza sura bali nipo kwa kazi moja tu nayo ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu na hilo halina ubishi kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu jambo hili linawezekana kwani tumetukanwa vya kutosha na mahasimu wetu Yanga,” alisema Kichuya.

Akielezea suala la kuumia kwake katika mchezo kati ya Simba na Mbeya City, Kichuya alisema anaendelea vizuri japokuwa daktari wa timu hiyo ya Msimbazi, Yassin Gembe, amedai kuwa staa huyo anaweza kuikosa mechi ijayo dhidi ya Kagera Sugar.

“Kichuya kaumia enka, tutajua ukubwa wa jeraha lake kesho (leo), kwa sasa ni mapema mno kufahamu iwapo atacheza mechi ijayo dhidi ya Kagera Sugar, kwa ufupi ni 50/50 anaweza kuwa fiti au asiwe fiti kufikia kwenye mechi hiyo,” alisema Gembe.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -