Tuesday, January 19, 2021

Kichuya afunga… Bao la rekodi duniani

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA HASSAN DAUDI,

MOJA kati ya mabao matamu yaliyowahi kutokea katika mchezo wa mahasimu Simba na Yanga ‘Kariakoo derby’ ni lile lililofungwa juzi na staa Shiza Kichuya.

Katika mtanange huo ambao timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, Kichuya ndiye aliyeisawazishia Simba, baada ya Amis Tambwe kuitanguliza Yanga katika dakika ya 26.

Kichuya alifunga bao hilo kwa mpira wa kona uliokwenda moja kwa moja kwenye nyavu za Yanga.

Kama ulikuwa hujui, wataalamu wa soka wanalitambua bao hilo kwa jina la ‘Olympic goal’. Ni wazi kuwa ni nadra kushuhudia aina ile ya mabao.

Unaweza kujiuliza, kwanini bao la aina hiyo lilipachikwa jina hilo la Olympic goal?

Jibu ni kwamba, aliyekuwa straika wa Argentina, Cesareo Onzari, ndiye aliyekuwa mchezaji wa kwanza kufunga kwa staili ya Kichuya katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Uruguay, uliochezwa mwaka 1924.

Kulikuwa na taarifa kuwa mwaka 1923 Billy Alston wa Scotland alifunga aina hiyo ya mabao, lakini uchunguzi ulibaini kuwa mpira wake wa kona uliguswa kabla ya kutinga wavuni. Hivyo, Onzari alibaki kuwa mwanzilishi wa Olympic goal.

Wakati Onzari anapachika bao hilo kwa mpira wa kona uliotokea upande wa kushoto, Argentina ndio waliokuwa mabingwa wa michuano ya Olimpiki.

Kutokana na hilo, kuanzia hapo, bao lililotokana na mpira wa kona bila kuguswa na mchezaji mwingine ‘lilibatizwa’ jina la Olympic goal.

Mwingerza wa kwanza kuingia kwenye historia ya kufunga Olympic goal alikuwa Billy Smith, aliyekuwa akikipiga katika klabu ya Huddersfield Town.

Lakini, aina hiyo ya mabao haikuwa ikikubalika mpaka pale Bodi ya Chama cha Soka cha Kimataifa ilipokutana kujadili na kisha kuruhusu katika siku za baadaye.

Mwanasoka anayeshikilia rekodi ya kufunga Olympic goal mara nyingi ni Sukru Gulesin wa Uturuki.

Kwa kipindi chote cha maisha yake ya soka, Mturuki huyo alipachika Olympic goal mara 32.

Mwaka 1950, nyota huyo aliingia kwenye Kitabu cha Kumbukumbu cha Guinness kutokana na idadi yake hiyo ya mabao.

Bao la kwanza la Olympic goal kufungwa kwenye fainali za kombe la dunia ni la mwaka 1962, lililowekwa wavuni na Marcos Coll wa Colombia.

Wakati wa michuano ya Kombe la Washindi barani Ulaya ya mwaka 1964, Mreno Joao Morais alifunga Olympic goal wakati akiichezea timu yake ya Sporting Clube.

Lakini pia, hata nahodha wa zamani wa timu ya Taifa wa England, David Beckham, aliwahi kufunga mabao kadhaa kwa staili hiyo.

Mwaka 2012, akiwa na New York Red Bulls ya Marekani, Mfaransa Thierry Henry alipiga mpira wa kona ambao haukuguswa na mchezaji mwingine kabla ya kutinga nyavuni.

Ni kipindi hicho ndipo Megan Rapinoe wa timu ya soka ya wanawake ya Marekani alipofunga Olympic goal katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Olimpiki iliyofanyika jijini London.

Kwa kufanya hivyo, mwanadada Megan alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga Olympic goal katika michuano hiyo.

Jinsi ya kuzuia kona

Imezoeleka kuona washambuliaji wa timu ya mchezaji anayepiga kona wakisogea kwenye goli la timu pinzani kulazimisha mipira ya vichwa.

Timu inayojiandaa kuokoa mashambulizi, huweza kuweka ‘ukuta’ ili kuzuia mpira wenye madhara langoni mwao.

Kwa kuweka ukuta, watalazimisha mpira wa kona kutua mahali ambako ni rahisi kwao kuokoa.

Lakini pia, huenda timu inayopigiwa kona ikaamua kuwatumia wachezaji wawili kusimama kwenye ‘posti’ ya goli ili kuokoa mpira ambao unaweza kumpita mlinda mlango wao.

Mara nyingi, hata barani Ulaya, tumekuwa tukishuhudia jinsi gani mabeki wamekuwa wakiokoa mabao ya wazi kwa mtindo huo.

Mbinu nyingine ni ile ya timu inayopigiwa kona kuondoa baadhi ya wachezaji wake kwenye safu ya ulinzi.

Hii itakuwa na manufaa makubwa ikiwa wataupata mpira uliopigwa kona, kwani utawarahisishia shambulizi la kushitukiza ‘counter-attack’.

Hilo litatokana na ukweli kwamba wachezaji wengi wa timu inayoshambulia watakuwa langoni mwao, hivyo kuacha mapengo katika safu ya kiungo na hatimaye ile ya ulinzi.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -