Saturday, November 28, 2020

SHIZA KICHUYA AISHTUA SIMBA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SAADA SALIM


UKWELI ni kwamba Simba imeshtuka baada ya kugundua kwa sasa inamtegemea zaidi winga wao, Shiza Ramadhani ‘Kichuya’, katika kupachika mabao kitu ambacho si sahihi endapo atakosekana kikosini kwa sababu yoyote ile.

Kwa kuliona hilo na kwakutambua kwamba washambuliaji wengine hasa wa kigeni wameshindwa kufikia matarajio, Wekundu hao wameingia mtaani kusaka straika mwingine mzawa wakiamini wanaweza kumpata na akafanya mambo makubwa kama ilivyo kwa Kichuya.

Kichuya aliyesajiliwa na Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, ndiye kinara wa ufungaji ndani ya kikosi cha Simba na hata katika Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa amefumania nyavu mara tisa.

Kocha wa Simba Mcameroon, Joseph Omog, ameliambia BINGWA kuwa ameiagiza kamati ya usajili ya klabu hiyo kuhakikisha inafanikisha kusajiliwa kwa mshambuliaji mwenye ubora ambaye atachochea ushindani na wapachika mabao wengine wa timu hiyo Mrundi, Laudit Mavugo na raia wa Ivory Coast, Frederick Blagnon.

Washambuliaji hao wa kigeni wameonekana kutokidhi mahitaji ya benchi la ufundi ambalo kwa sasa wamekuwa wanamtegemea zaidi Kichuya.

Hatua hiyo ya Omog ni dhahiri imechangiwa kupungua kwa ufanisi katika kikosi chake ambacho kilishuhudiwa kikipoteza mechi mbili mfululizo za mzunguko wa kwanza ambacho kilichapwa bao 1-0 na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kisha kucharazwa mabao 2-1 na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

“Jukumu la usajili lipo chini ya kamati inayohusika, mimi nilichofanya ni kushauri nini kifanyike ili Simba iweze kufanya vizuri zaidi mzunguko wa pili na kutwaa ubingwa,” alisema Omog.

Akizungumzia tathmini ya uwezo wa kipa Daniel Agyei, kocha huyo alisema ameridhishwa na ubora wake, lakini ataendelea kumfuatilia kwa makini kupitia mazoezi na mechi za kirafiki ambazo kikosi chake kinatarajia kucheza.

“Usajili unaendelea chini ya kamati husika, tayari wameshaanza kwa kipa naamini watafuata kile nilichokihitaji katika ripoti yangu, suala la kipa nahitaji kumwona katika mazoezi na kwenye mechi za kirafiki.

“Ili kujiweka fiti zaidi kwa ajili ya mzunguko wa pili, pia tunatarajia kucheza mechi kadhaa za kirafiki ambazo pia nitazitumia kupima viwango vya wachezaji wapya kwenye kikosi,” alisema kocha huyo wa zamani wa Azam FC.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -