Monday, January 18, 2021

KICHUYA ‘APORWA’ MABAO MSIMBAZI

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAINAB IDDY

LICHA ya kutumia zaidi ya dakika 200 uwanjani na kushindwa kucheka na nyavu, benchi la ufundi la Simba limemkingia kifua kiungo wao mshambuliaji, Shiza Kichuya, baada ya kusema kuwa hakwenda katika kikosi hicho kwa kazi hiyo bali kuisaidia timu iweze kupata matokeo mazuri.

Tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, Kichuya akiwa akianzishwa kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Joseph Omog, ameshindwa kwenda na kasi yake ya upachikaji mabao kama ilivyokuwa kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.

Kwenye mzunguko wa kwanza, Kichuya aliifungia mabao tisa timu yake ambayo tayari yameshafikiwa na mastraika wa Yanga,  Amissi Tambwe pamoja na Simon Msuva.

Akizungumza mara baada ya mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting uliomalizika kwa Simba kushinda 1-0, kocha msaidizi wa Wekundu wa Msimbazi, Jackson Mayanja, alisema awali Kichuya alipokuwa Mtibwa hakuwa anafunga mara kwa mara kama iliyokuwa baada ya kusajiliwa na Wanamsimbazi hao.

“Nina hakika waliokuwa wanamfahamu Kichuya watakubaliana na mimi kuwa hakuwa mfungaji kama ilivyo hivi sasa Simba, hivyo tunachohitaji sisi ni kuona mchango wake katika kuipa mafanikio timu pasipo kujali amefunga au la.”

Wakati Mayanja anasema hayo, Kichuya amefunguka kuwa moja ya vitu vinavyosababisha kushindwa kucheka na nyavu katika mzunguko huu ni kukamiwa na wapinzani wao.

Alisema tangu kuanza ligi msimu huu mabeki wengi wamekuwa wakimkamia zaidi yeye jambo linalomnyima upenyo wa kucheka na nyavu za wapinzani na hivyo kulazimika kuwapa pasi wenzake ili waweze kufunga na hatimaye Simba kuibuka na ushindi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -