Sunday, October 25, 2020

KICHUYA ATAWAKIMBIA TAMBWE, MSUVA LEO?

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA EZEKIEL TENDWA

WINGA wa Simba, Shiza Kichuya, ameongoza kwa muda mrefu katika orodha ya wafungaji msimu huu lakini ghafla akajikuta akilingana na Amis Tambwe na Simon Msuva wa Yanga, ila ana fursa ya kuwakimbia washindani wake hao kama atafanikiwa kupachika bao katika mchezo dhidi ya Azam.

Kichuya anayo mabao tisa sawa na Tambwe na Msuva, lakini kama leo atafunga Wekundu hao wa Msimbazi watakapowakabili Azam FC Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, atakuwa amewatoroka kiaina.

Hata hivyo, kama atashindwa kufunga leo na kesho Msuva au Tambwe akafunga Yanga watakapowakabili Mwadui FC, uwanja huo wa Uhuru, ni wazi Kichuya ataachwa kwenye mataa.

Kichuya ambaye alisajiliwa na Simba kutoka kwa wakata miwa wa Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro, alianza kwa kishindo akifunga mabao muhimu lakini ghafla kasi yake hiyo ikapungua na kujikuta akilingana na Msuva na Tambwe.

Moja ya mabao muhimu aliyoyafunga Kichuya ni pamoja na lile la kusawazisha la dakika za lala salama dhidi ya Yanga akifunga kwa ufundi mkubwa kwa njia ya kona na mpira kujaa wavuni moja kwa moja na kumalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Pia bao jingine lililowafanya mashabiki wa Simba kuondoka uwanjani kwa furaha, ni lile dhidi ya Azam FC akiachia shuti kali lililomshinda kipa Aishi Manula na Wekundu hao wa Msimbazi kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -