Tuesday, October 20, 2020

Kichuya: Kuondoka Simba ‘fresh’ tu

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA ZAINAB IDDY

WINGA Shiza Ramadhani ‘Kichuya’, amesema yupo tayari kuondoka Simba na kwenda kucheza soka la kulipwa iwapo  Klabu ya Chippa United ya Afrika Kusini itamhitaji.

Klabu ya Chippa United imevutiwa na Kichuya baada ya kuonyesha uwezo wa hali ya juu wa kucheza soka Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambaye kwa sasa anaongoza kwa kufunga mabao saba.

Akizungumza na BINGWA jana Kichuya alisema malengo ni kutaka kucheza soka ya kulipwa nchi ya Tanzania kama ilivyo kwa Mbwana Samatta  anayekipiga Genk ya Ubelgiji na Thomas Ulimwengu, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Kichuya alisema  hawezi  kuikataa ofa itakayokuja mbele yake  lakini wanaomhitaji ni lazima wazungumza na wakala wake na Simba  kwani bado ana mkataba na klabu hiyo.

“Nipo tayari kwenda kucheza soka nchi yoyote ili niweze kutimiza malengo yangu, lakini inafahamike kuwa mimi si mchezaji huru nina mkataba na Simba,” alisema Kichuya.

Alisema licha ya kwamba ana mkataba na Simba, lakini kwa kushirikiana na meneja wake ni lazima waangalie aina ya ofa inayokuja, kwani nyingine zimekaa kiujanja ujanja.

“Unajua si kila ofa unaitolea macho na kuikubali kwani mjini hapa ujanja mwingi, kikubwa ni kukaa mezani baina ya meneja wangu, uongozi wa Simba na hao watakaonihitaji kuona kuna masilahi gani kwangu.”

Kichuya alijiunga na Simba msimu huu wa ligi kuu kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mtibwa Sugar aliyoitumikia kwa takribani misimu mitatu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -