Tuesday, October 20, 2020

KICHUYA, MO IBRAHIM WAWEKEWA MTEGO MORO

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA WINFRIDA MTOI

SIMBA licha ya kujenga kombinesheni nzuri ya washambuliaji wake, Mtibwa Sugar imeweka mtego maridadi kuwakwamisha vinara hao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania kama watapanga kuwatumia winga, Shiza Kichuya na kiungo mshambuliaji, Mohammed Ibrahim ‘Mo’.

Wawili hao pamoja na Mzamiru Yassin wote wametokea Mtibwa Sugar, hivyo miamba hao wa Manungu wamejipanga vyema, ikiwa ni sambamba na kuwategea mitego nyota hao wa Simba katika mchezo wao wa keshokutwa, kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro.

Akizungumza na BINGWA jana, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, alisema pamoja na Kichuya na MO kuwa ni wachezaji wazuri ambao wanasumbua mabeki wengi wa Ligi Kuu Bara, wao Mtibwa wanajua udhaifu wao, lakini pia  kikosi kizima cha Simba.

Kifaru alisema ana uhakika timu yao itaibuka na ushindi, kwani watatumia udhaifu wa wachezaji wao waliosajiliwa na Simba, akiwamo Mzamiru Yassin, Juma Luizio, MO na Kichuya.

Alisema wachezaji  hao wanne wanatisha katika kikosi cha Simba wanatokea kwenye timu yao, hivyo wanajua ubora na udhaifu  wao, kwani kocha wao tayari wamewapa maelekezo wachezaji wake jinsi ya kuwadhibiti.

“Ili kupata ushindi kwa Simba lazima tukaze sana, ila tunachojivunia wachezaji wanne  wa kikosi hicho ambao tumewalea wenyewe na tunajua udhaifu wao na ndio tutakaowatumia kupata matokeo mazuri,” alisema Kifaru.

Alisema pamoja na kiwango cha wachezaji kuonekana kuwa kipo juu, lakini hawatishwi  na lolote, kwani wana silaha nyingine walizotengeneza ambazo watazitumia kwa ajili ya maangamizi.

“Tunaiheshimu Simba kutokana na kushikilia usukani kwenye msimamo wa ligi, mwalimu wetu anafanya maandalizi ya kutosha ili kuibuka na ushindi, ila tunasikitika tunaweza tukamkosa  Salim Mbonde aliyepata majeraha ya mguu wakati wa mazoezi,” alisema Kifaru.

Simba tayari wamewasili mkoani Morogoro wakitokea visiwani Zanzibar ambao wamekwenda kushiriki Kombe la Mapinduzi na kushindwa kuchukua ubingwa, baada ya kufungwa bao 1-0 na Azam katika mchezo wa fainali iliyochezwa Ijumaa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Amaan.

Previous articleNGOMA KUIKOSA SIMBA
Next articleAZAM FC YAPATA JEURI
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -