Wednesday, October 28, 2020

KICHUYA: MO NJOO TAIFA UFURAHI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA GLORY MLAY


 

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya, amewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo, akiwamo mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji ‘Mo’, kufika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Jumapili bila wasiwasi wowote, kwani hatawaangusha.

Simba wanatarajiwa kuwa wenyeji wa watani wao wa jadi, Yanga, katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambao ni wa kwanza kwa msimu huu.

Akizungumza na BINGWA jana, Kichuya alisema  mchezo huo ni kama ilivyo mingine, hivyo anamuomba Mungu awe na afya njema ili atimize kile wanachokitaka mashabiki na wanachama wa Simba.

Alisema yupo fiti na amejiandaa vema kuhakikisha anaendeleza rekodi yake ya kufanya kile ambacho amekuwa akikifanya kila wanapokutana na Yanga.

“Nina bahati ya kuifunga au kusababisha bao tunapokutana na Yanga, naamini rekodi hiyo itajirudia tena Jumapili, nawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi siku hiyo ili kushuhudia tukiibuka na pointi tatu,” alisema Kichuya.

Ikumbukwe Oktoba 1, 2016, Kichuya aliifunga Yanga kwa mara ya kwanza akiwa Simba, bao lake hilo likiwa ni la kusawazisha wakati timu hizo zilipotoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa.

Februari 25, 201

7, Kichuya akaifunga tena Yanga kwa mara ya pili mfululizo na kuiwezesha Simba kupata ushindi wa mabao 2-1 kwenye uwanja huo, kabla ya winga huyo kuisawazishia timu yake katika sare ya bao 1-1 Oktoba 28, mwaka huo dhidi ya Wanajangwani hao.

Katika mchezo uliopita ambao Simba ilishinda bao 1-0, Kichuya alitoa pasi ya bao hilo pekee lililofungwa na beki, Erasto Nyoni.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -