Monday, October 26, 2020

KICHWA CHA TAMBWE KATIKA MWILI WA KAGERE

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA SALMA MPELI


 

UKIWAZUNGUMZIA wakali wa kufunga mabao ya kichwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa miaka ya hivi karibuni, basi huwezi kuacha kutaja jina la straika wa Yanga, Amissi Tambwe.

Mchezaji huyo raia wa Burundi, aliingia kwa mara ya kwanza nchini msimu wa mwaka 2013/14, akisajiliwa na Wekundu wa Msimbazi, Simba, kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Vital’O ya Burundi.

Kwenye msimu wake wa kwanza akiwa na kikosi cha Simba, Tambwe aliibuka mfungaji bora, akitupia mabao 19 kwenye msimu huo.

Licha ya kuibuka mfungaji bora wa msimu, Simba walimtema Mrundi huyo mwaka uliofuata kwa kigezo cha kushuka kiwango baada ya kocha wake, Patrick Phiri, kuwaambia mabosi wa timu hiyo haendani na namna timu yake inavyocheza.

Tambwe alitemwa kwenye dakika za mwisho za kufungwa kwa dirisha la usajili wa ligi hiyo, lakini aliangukia kwenye mikono ya Wanajangwani kwa miaka mingine miwili. Wakati anaondoka Simba katika msimu huo, Tambwe alikuwa amefunga bao moja pekee, alipotua Yanga, alifanikiwa kufunga mabao 13.

Katika kuwadhihirishia Simba kwamba walifanya makosa kumwacha, straika huyo alifanikiwa kuibuka tena mfungaji bora msimu uliofuata akiwa Yanga kwa kufunga mabao 21 na kuisaidia timu hiyo kuibuka mabingwa wa Ligi Kuu Bara.

Asilimia kubwa ya mabao ya Mrundi huyo ni ya kichwa, ambako kwa sasa mastraika wanaoongoza kwa kufunga mabao ya kichwa, basi Tambwe anaongoza.

Wakati wadau wa soka nchini wakianza kuusahau ufalme wa mabao ya kichwa wa Tambwe, Simba imesajili mashine nyingine kutoka Gor Mahia ya Kenya.

Anaitwa Meddie Kagere raia wa Rwanda, lakini alikuwa akicheza kwenye Ligi ya Kenya ambako Simba walimuona na kushawishika na kiwango chake baada ya kuwafunga kwenye michuano ya SportPesa.

Simba walifungwa mabao 2-0 dhidi ya Gor Mahia katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo iliyofanyika nchini Kenya yaliyofungwa na Kagere kwa kichwa na Mrwanda Jacques Tuyisenge.

Mbali na bao lake hilo kwenye mchezo wa fainali, Kagere ambaye aliibuka mfungaji bora kwenye michuano hiyo akifunga mabao matano, huku matatu kati yao yakiwa ni ya kichwa, uwezo wake huo uliwafanya Simba kumng’oa mkali huyo kwenye kikosi cha Gor Mahia.

Tangu ametua Simba, Kagere amefunga mabao kadhaa kwenye mechi mbalimbali, ikiwa zile za michuano ya Kagame Cup iliyofanyika hapa nchini na mechi za kirafiki kwenye maandalizi ya msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Ligi Kuu Bara imeanza kutimua vumbi Agosti 22, mwaka huu, ambako Simba imecheza mechi mbili na kushinda zote huku ikijikusanyia pointi sita na mabao matatu.

Ushindi huo wa Simba katika michezo miwili umechangiwa na Kagere ambaye amefunga mabao yote hayo, moja akifunga kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons na mawili akifunga kwenye mchezo wa pili dhidi ya Mbeya City, zote zikichezwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Kagere ameanza kuonekana ni moto kwenye kikosi cha Simba na kuanza kutishia amani miongoni mwa wafungaji wa ligi hiyo ambayo msimu uliopita, Emmanuel Okwi alitwaa kiatu cha ufungaji bora akiifungia Simba mabao 20 na kuisaidia kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Mbali na kuingia kwenye orodha ya wafungaji bora msimu huu, Kagere amekuwa mkali zaidi katika kutupia mabao ya kichwa kama ilivyokuwa kwa Tambwe.

Katika mchezo wao dhidi ya Mbeya City, mabao yote mawili aliyofunga ni ya aina moja na yote akifunga kwa kichwa, moja akimalizia pasi ya Shiza Kichuya na jingine ya Asante Kwasi.

Kutokana na kasi anayokuja nayo straika huyo wa Simba kwa sasa ya aina yake ya ufungaji mabao kwa kichwa, ni wazi unaweza kumfananisha na Tambwe ambaye kwa miaka yote aliyocheza Ligi ya Tanzania ndiye aliyekuwa mfalme wa mabao ya vichwa.

Tangu amekosekana kwa muda katika kikosi cha Yanga kutokana na majeraha, Tambwe ameifanya timu hiyo kukosa kabisa mtu wa aina yake wa kuweza kufunga mabao ya aina hiyo.

Wafungaji wengine waliopo kwenye timu hiyo wanashindwa kuitendea haki mipira ya juu ambayo angekuwepo Tambwe ambaye msimu uliopita haukuwa mzuri kwake kutokana na majeraha ya mara kwa mara, basi angeendelea na staili yake.

Kwa sasa tunamtazama Kagere akitupia mabao hayo ambayo unaweza kusema ni Tambwe mpya katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -