Sunday, November 29, 2020

Mourinho kuzikosa Swansea, Arsenal

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

HUENDA Chama cha Soka cha England (FA) kikampa kocha, Jose Mourinho, adhabu ya kutokaa benchi la timu yake ya Manchester United, baada ya kutoa kauli za uchochezi kwa mwamuzi, Anthony Taylor.

Mourinho alidai kwamba mwamuzi huyo anayeishi jirani na Uwanja wa Liverpool, atashindwa kuchezesha vizuri mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool uliochezwa wiki iliyopita.

Mourinho alikuwa akifafanua uamuzi wa mwamuzi huyo anayeishi jirani na Uwanja wa Old Trafford kupewa jukumu la kuchezesha mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa sare ya 0-0 katika Dimba la Anfield.

FA imemkuta Mourinho na hatia, hivyo huenda akapewa adhabu ya kutokaa kwenye benchi la timu yake kwa mechi kadhaa na atapigwa faini na amepewa muda hadi Oktoba 31 mwaka huu, kutoa maelezo juu ya kauli yake.

Mourinho alisema hataki kusema lolote kwa kuwa amejifunza mengi baada ya kupewa adhabu mara kadhaa kuhusiana na kauli zake kuhusu waamuzi.

“Taylor ni mwamuzi mzuri, lakini nafikiri atakuwa kwenye hofu kutokana na kelele za watu wanaodai atachezesha vibaya kwa kuwa ametokea Mji wa Manchester. Hivyo, nahisi itakuwa ngumu kwake kuchezesha vizuri,” alisema kocha huyo wa Ureno.

Mourinho anajua kwamba waamuzi hawaruhusiwi kuzungumza kabla ya mechi.

Hivyo kama atafungiwa mechi mbili kwa kosa hilo, Mourinho ataukosa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Swansea utakaochezwa Novemba 6 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Liberty na mechi nyingine itakuwa ni Novemba 19 mwaka huu, dhidi ya Arsenal itakayopigwa Old Trafford.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -