Tuesday, October 27, 2020

KIGOGO YANGA AWATULIZA PRESHA WACHEZAJI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR

KIGOGO wa Yanga mwenye uwezo mkubwa wa kifedha amewataka wachezaji wao kutuliza presha, baada ya Simba kufungwa bao 1-0 na Azam, kwani taji la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu litaendelea kubaki Mtaa wa Twiga na Jangwani.

Akizungumza na BINGWA jana, kigogo huyo ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya mashindano ya klabu hiyo,  alisema baada ya Simba kuchemka sasa ubingwa ni njia  mweupe kwao.

Mjumbe huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema wanaendelea na mipango ya kuiwezesha timu yao kutetea ubingwa wao, kwani wachezaji wanatakiwa kutuliza akili zao na  kutafuta pointi tatu.

“Muda mrefu tulitamani wapinzani wetu Simba wapoteze, wateleze sisi tushinde. Elewa kuwa ligi ya msimu huu ni ngumu na niwaombe wachezaji watulize akili zao na waondoe presha ya ubingwa. Muhimu watafute pointi tatu kwanza kabla ya kufikiria ubingwa,” alisema bosi huyo.

Alisema mambo mengi yatatokea katika kipindi hiki ambacho ligi kuu inaelekea ukingoni, ikiwamo kuondolewa mchezoni na waamuzi na hata kufanyiwa fitina na timu pinzani.

“Naomba wachezaji wetu wadumishe nidhamu, waepuke kupata kadi ambazo hazina ulazima, kwani tumedhamiria kuubakisha ubingwa Jangwani. Naweza kusema bado tuna kazi kubwa mbeleni ndio maana nawaambia waache kufikiria kuongoza ligi badala yake wahakikishe wanapata ushindi katika kila mchezo.”

Kigogo huyo alilisitiza kuwa wao kama kamati ya mashindano wamekuwa wakijitahidi kadiri ya uwezo wao kuhakikisha wanawaongezea hamasa wachezaji wa timu hiyo ili waweze kupata ushindi uwanjani katika kila mchezo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -