Sunday, November 1, 2020

Kiiza acheza dakika tisa Sauzi

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU,

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Hamis Kiiza, mwishoni mwa wiki iliyopita alicheza kwa dakika tisa tu wakati kikosi chake cha Free State Stars kilipolazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Highlands Park, mchezo wa Ligi Kuu nchini Afrika Kusini.

Katika mchezo huo ambao kikosi hicho cha Free State kilikuwa ugenini, Kiiza aliingia dakika ya 81 yaani zikiwa zimebakia dakika tisa mchezo kumalizika akichukua nafasi ya Nyiko Mobbie.

Matokeo hayo ya sare yanazidi kukiweka katika hali ngumu kikosi hicho cha akina Kiiza kwani kipo nafasi ya 14 kati ya timu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya nchini Afrika Kusini.

Katika ligi hiyo, Free State wamecheza michezo saba ambapo kwenye michezo hiyo kikosi hicho hakijafanikiwa kushinda hata mchezo mmoja kikitoka sare michezo minne na kufungwa mitatu kikiwa na pointi nne.

Kiiza amesajiliwa na kikosi hicho kuziba pengo lililoachwa wazi na winga machachari wa kulia Mtanzania, Mrisho Ngassa, aliyeamua kwenda kucheza soka nchini Oman.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -