Tuesday, November 24, 2020

Kiiza amfunika Ngassa Sauz

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA EZEKIEL TENDWA,

STRAIKA wa zamani wa Simba, Mganda Hamis Kiiza, amekuwa tegemeo katika Klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini, kutokana na kuwa kikosi cha kwanza, licha ya ugeni wake tofauti na Mrisho Ngassa, aliyeamua kutimka zake kikosini hapo.

Ngassa, ambaye ni winga wa zamani wa timu za Yanga, Simba pamoja na Azam FC, ameamua kuachana na timu hiyo kutokana na kukosa namba ya kudumu ambapo kuondoka kwake kulimpa nafasi Kiiza kusajiliwa.

Tangu kusajiliwa kwa Ngassa ilikuwa mara chache sana kuanza kikosi cha kwanza, kwani mara nyingi alikuwa akitokea benchi na sasa ameamua kuvunja mkataba na kutimkia Fanja FC ya nchini Oman.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa Ngassa, kwa upande wa Kiiza, ambaye amesajiliwa kuchukua nafasi ya Mtanzania huyo, ameanza kikosi cha kwanza katika michezo yote minne ambayo timu yake hiyo imecheza.

Kiiza alianza katika mchezo dhidi ya Bloemfontein Celtic, uliochezwa Septemba 14, mwaka huu, uliomalizika kwa suluhu ya 0-0, ambapo alicheza dakika zote 90, ikiwamo pia mchezo dhidi ya Golden Arrows, walipokubali kichapo cha bao 1-0.

Pia alicheza dakika zote 90 mchezo dhidi ya SuperSports United, uliomalizika kwa suluhu ya 0-0 na pia akacheza kwa dakika 68 mchezo uliopita dhidi ya Kaizer Chiefs, uliomalizika kwa Free State kukubali kichapo cha mabao 2-0.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -