Tuesday, October 27, 2020

Kiiza katika kibarua kigumu Sauzi leo

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba Mganda, Hamis Kiiza, leo ndiyo kipimo cha uwezo wake kitakapoonekana kikosi chake cha Free State kitakapoikabili timu ngumu ya SuperSport United.

Kikosi hicho cha Free State Stars kitakuwa ugenini katika Uwanja wa King Zwelithini Stadium, dhidi ya wapinzani wao hao ambapo Kiiza anatarajiwa kuonyesha uwezo wake ili kudhihirisha kuwa hakusajiliwa kwa bahati mbaya.

Kiiza ambaye alisajiliwa na kikosi hicho akitokea Simba ambao walimtema kwa madai ya utovu wa nidhamu, alianza kuitumikia timu yake hiyo mpya katika mchezo dhidi ya Bloemfontein Celtic, uliomalizika kwa suluhu ya 0-0.

Mganda huyo amesajiliwa baada ya kikosi hicho kufikia maamuzi ya kuvunja mkataba na Mtanzania, Mrisho Ngassa, ambaye kwa sasa ameamua kutimkia nchini Oman kukipiga klabu ya Fanja.

Katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Afrika Kusini, kikosi hicho cha Free State Stars anachochezea Kiiza kinashika nafasi ya pili kutoka mkiani kikiwa na pointi moja katika michezo mitatu waliyokwisha kucheza mpaka sasa wakifungwa miwili na kutoka sare mmoja.

Kwa upande wa wapinzani wao SuperSport United, wanashika nafasi ya tisa wakiwa na pointi nne katika michezo mitatu waliyocheza wakishinda mmoja, sare mmoja na kupoteza mchezo mmoja ambapo Orlando Pirates, wanaongoza wakiwa na pointi saba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -