Friday, November 27, 2020

KILA LA KHERI BARA, ZANZIBAR JUDO A/MASHARIKI NA KATI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MICHUANO ya Afrika Mashariki na Kati kwa mchezo wa judo inatarajiwa kuanza leo visiwani Zanzibar, huku vikosi vya timu za Tanzania Bara na Zanzibar vikipewa nafasi kubwa ya kutwaa medali za kutosha.

Michuano hiyo inashirikisha nchi saba ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Tanzania Bara na wenyeji Zanzibar.

BINGWA tukiwa wadau wakubwa wa michezo kwanza tunaipongeza Zanzibar kwa kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo, kwani ni fursa ya kujiweka vyema kutimiza ile methali isemayo mcheza kwao hutunzwa.

Tunaamini kwa muda mrefu vikosi vya timu za Zanzibar na Tanzania Bara vimejiandaa vya kutosha kuitoa kimasomaso Tanzania kwenye michuano hiyo na kuiweka kwenye ramani bora kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Kwa nyakati tofauti makocha wa timu hizo wamekwishaeleza kuwa timu zao ziko kwenye morali ya hali juu baada ya kujiandaa kwa muda mrefu na hivyo hawana wasiwasi katika ushiriki wao.

Tunasema itakuwa ni aibu kwa Tanzania kuvurunda kwenye michuano hiyo na kuwapa nafasi wageni waondoke na medali katika ardhi ya nyumbani. Wachezaji wa timu hizo wanapaswa kuingia katika michuano hiyo wakiwa na kauli mbiu kwamba, hakuna cha kuwazuia wasitwae medali zote wao ikiwa wana kila sababu ya kufanya hivyo.

Ni imani yetu hakutakuwa na visingizio vya kushindwa kufanya vyema ikiwa nyota wa timu walishajengwa kiufundi na kisaikolojia kabla ya kipenga cha kuanza kwa michuano hiyo hakijapulizwa.

Wachezaji wa timu hizo wajue mamilioni ya Watanzania wako nyuma yao wakiwaombea dua ili watakate, lakini nao wafahamu wajibu walionao uwanjani katika mapambano ya kuwania medali.

BINGWA tunamalizia kwa kusema tunazitakia kila la kheri timu hizo tukiamini medali zote za michuano hiyo zinapaswa kubaki katika ardhi ya Tanzania.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -