Monday, November 30, 2020

KILA LA KHERI WAWAKILISHI WETU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga, Zimamoto na KVZ, leo zina kibarua kigumu pale zitakapopeperusha bendera ya nchi katika viwanja tofauti ndani na nje ya nchi.

Yanga ya Tanzania Bara itakuwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikipambana na Ngaya de Mbe ya Comoro wakati KVZ ya Zanzibar wao watakua ugenini katika Uwanja wa Rwagasore mjini Bujumbura, nchini Burundi.

Mechi hizo ni za Ligi ya Mabingwa barani Afrika na ni muhimu kwa timu hizo ili ziweze kusonga mbele hatua inayofuata katika safari yake ya kuwania ubingwa huo wenye hadhi ya juu kabisa barani humo.

BINGWA tunawakumbusha wawakilishi hao wa Tanzania kutambua wazi kuwa mchezo huo ni muhimu kwao kwa vile mbali ya kujipatia sifa pamoja na nafasi ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo vile vile wanaitangaza nchi.

Wawakilishi hao wanapaswa kutambua ushiriki wao ni nafasi pekee ya kuitangaza nchi katika anga la kimataifa kupitia fani ya michezo.

Timu hizo zitambue ushindi wa mechi za leo ni hatua muhimu kwao katika harakati za safari ya kuwania kutwaa ubingwa wa Afrika.

BINGWA tuna imani timu zote zina uwezo wa kusonga mbele kwani zilionesha viwango vya juu katika mechi zao za awali hivyo wanaingia katika mechi za leo wakiwa na mtaji wa mabao ya kutosha.

Katika mechi ya kwanza Yanga ikiwa ugenini iliifunga Ngaya mabao 5-1 wakati KVZ ilishinda kwa jumla ya mabao 2-1 mjini Zanzibar sawa na Zimamoto.

Tunatoa wito kwa mashabiki wote wa soka nchini kuweka kando itikadi za klabu zao na kusimama kwa pamoja kutoa sapoti ya nguvu kwa Yanga ikiwa jijini Dar es Salaam sambamba na kuiombea KVZ ikiwa mjini Bujumbura.

BINGWA inaungana na Watanzania wote kuzitakia kila la kheri timu hizo ili zitimize ndoto zao na kututoa kimasomaso.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -